HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 26, 2012

MSHINDI DROO KUBWA MZUKA WA AIRTEL AKABIDHIWA ZAWADI YAKE MILIONI 50 MKOANI MBEYA

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw Jackson Mbando akimkabidhi bw Peter Lucas Laizer ambae ni mkazi wa Dodoma mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 ikiwa ni zawadi yake aliyojishindia wakati wa droo ya mwisho ya promosheni ya MZUKA wa Airtel iliyosha hivi karibuni. Katikati anaeshudia ni ofisa huduma kwa wateja mkoa wa Mbeya Bw Hamfrey George. Airtel imekabidhi mfano wa hundi hiyo mwishoni mwa wiki kwa dhamira ya kujulisha wateja wake tayari mshindi huyo ameshawekewa hela zakekatika akaunti yake
Kulia ni Ofisa huduma kwa wateja wa Airtel mkoani mbeya Hamfrey George na kushoto Giliadi Mshana wakimpongeza kwa namna ya kipekee bw Peter Lucas Laizer ambae ni mkazi wa Dodoma na pia mshindi wa droo ya kubwa ya mzuka wa airtel aliyejishindia shilingi milioni 50 za Airtel. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani mbeya ambapo mshindi huyo yuko huko kikazi na Airtel ilifanya hivyo kwa dhamira ya kujulisha wateja wake wote kuwa tayari mshindi huyo ameshawekewa hela zakekatika akaunti yake
Bw. Peter Lucas Laizer mkazi wa Dodoma na mshindi wa droo ya kubwa ya mzuka wa airtel aliyejishindia shilingi milioni 50 za Airtel akiongea na wanahabari mkani mbeya wakati wa hafla ya kukabidhiwa zawadi yake mwishoni mwa wiki. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani mbeya ambapo mshindi huyo yuko huko kikazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad