HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 9, 2012

MGOGORO BAINA YA MASAI WANAOPENDA TOHARA KWA NJIA YA KIENYEJI NA KANISA UMEKWISHA KATIKA ENEO LA ELERAI

Na Mery Ayo,Arusha

HATIMAYE ule mgogoro ambao ulikuwepo baina ya vijana wa kabila la kimasai na waumini wa kikristo katika eneo la Elerai wa kuwatembeza mitaani baadhi ya waumini ambao wanapingana na mila hiyo umekwisha na badala yake wamefanikiwa kuweka misimamo ambayo haitaweza kuwaumiza jamii ya kikristo pamoja na kabila la wa masai.

Muafaka huo ulifanikiwa kufikiwa mapema jana katika eneo la Elerai ambapo pande zote mbili ambazo zilikuwa zinakinzana kuhusiana na mila ya Tohara kwa njia za kienyeji hali ambayo ilisababisha watu wengi kutembezwa mitaani wakiwa watupu

Akiongea katika kikao hicho mzee wa boma la kimasai, Bw Labani Konina laizer Alisema kuwa mila hizo zinawakandamiza sana baadhi ya watu ambao ni wa kabila hilo ambao hawaamini kwa maana hiyo ni bora mila kama mila ibaki kama iliuvyo na wala si lazima kufuatwa

Aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa matukio mengoi ya kutembezwa umbali mrefu kwa wale ambao wanakinzana na tohara za kienyeji familia nying sana zimekuwa katika wakati mgumu sana ambapo kwa sasa ni bora kanisa kama kanisa liwe na msimamo dhidi ya mila na pia anayetaka mila pia asibugudhiwe na mtu

"jamani kilichotokea ndugu tusamehane lakini hapa ni kwamba mtu asiingilie imani ya mtu kwa kuwa unapojaribu kuingilia imani ya mtu ndipo yanapotokea matatizo kama haya ya kutembezwa mitaani wakiwa watupu na pia hapa anayekwenda kanisa wazee wenzangu tuwaache na anayekuja huku aje lakini na sisi pia tuweze kuangalia mila ambazo hazina umuhimu kwetu tunapeleka wapi nchi"alisema Bw Laizer

Akiongea kwa niaba ya viongozi wa makanisa ya kikristo ambao walikuwa wanapinga na kukataa mila hiyo Bw Noel Urio alisema kuwa walichokubaliana wao kama wao ni kuhakikisha kuwa wana simama katika ukweli ambao utaweza kuokoa jamii hasa ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuachana na kuabudu mila ambazo zina madhara makubwa sana

Bw Noel aliongeza kuwa kwa sasa jamii ya kimasai ambayo ipo ndani ya madhehebu mbalimbali haitaweza kubugudhiwa dhidi ya Mila hiyo ambayo hapo awali ambao walikuwa hawaifuati walikuwa wanapewa adhabu kubwa sana ambayo inawapelekea kuwadhalilisha wao na familia zao.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata hiyo ya Elerai Bw Obedi Meng'oriki alisema kuwa bado mila hiyo ya Tohara kwa njia ya kienyeji ina dhalilisha sana kwa hali hiyo jamii hiyo ya Kimasai inatakiwa kuangalia hata hali ya Maisha ya sasa na kuachana na mila ambazo zimepitwa na wakati.

Bw Obedi aliongeza kuwa bado kuna watu ambao wana nganinia mila za hapo zamani na kutokana na wao kungangania mila hizo wamekuwa chachu ya umaskini ndani ya jamii zao hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana hata familia zao kuteseka sana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad