Jumuiya ya Wanafunzi wasomao na kuishi Bangalore, India, ilifanya mahafali yake mwishoni mwa wiki ambapo jumla ya wahitimu 49 walihitimu masomo yao mbali mbali ya degree za kwanza kwa wahitimu 39 katika nyanja za sheria, biashara, biotechnology, uhasibu, computer application na computer science na jumla ya wahitimu 10 walihitimu degree za pili za sheria, biashara, uchumi na uhasibu.
Mahafali hayo yalihudhuriwa na wageni mbali mbali waalikwa wakiwemo viongozi wa jumuiya za wanafunzi za nchi zingine zikiwemo za wa Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, South Africa, Chad, South Sudan, Ethiopia, Yemen, Ivory Coast, Zimbabwe na Sri Lanka.
Mara baada ya kutunukiwa nondoz zao, shughuli ilifuatiwa kwa msosi wa dinner wa kufa mtu, na baada ya hapo kukawa na dansi la kujipongeza lililosimamiwa vilivyo na Dj mkali kuliko wote Bangalore kutoka Kenya, Dj Charlie, Ambapo kwa maneno ya wengi ni kuwa hakujawahi kutokea sherehe nzuri iliyoandaliwa na jumuiya yoyote ya wanafunzi hapa Bangalore kama hiyo.
Wahitimu, walipongezwa na kuombewa maisha mema popote watakapoenda na wakatumie elimu zao walizozipata vyema.
Uongozi TASABA ( Tanzania Students' Association of Bangalore )
No comments:
Post a Comment