Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar,Dk. Sira Ubwa Mwamboga (kulia) akipokea msaada wa madawa ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya madawa ya kijerumani iitwayo Merck Dr. Karl Ludwig Kley
Mwanafunzi wa Skuli ya Ngwachani iliyopo Zanzibar,Selemani Sareh akinywa dawa ya kichocho kuashiria uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa huo iliyozinduliwa na Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar,Dk. Sira Ubwa Mwamboga (mwenye kiremba).kushoto kwake ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya madawa ya kijerumani iitwayo Merck Dr. Karl Ludwig Kley
Na Mwandishi Wetu
ASILIMIA 20 ya wakazi wa kisiwa cha Pemba wanakabiliwa na ugonjwa wa Kichocho katika mkojo.
Hayo yalibainishwa na naibu waziri wa afya wa Zanzibar Dk Sira Ubwa Mwamboga katika hafla ya kupokea msaada wa vifaa vya maabara kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo vilivyotolewa na kampuni ya madawa ya kijerumani iitwayo Merck.
Sira alisema kuwa ugonjwa umekuwa ukiwaathiri zaidi watoto wengi wao wakiwa ni wanafunzi ambao hutumia muda mwingi kucheza katika mito.
Alisema kuwa wizara yake kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya wamekuwa wakitoa elimu kwa wanajamii juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Alisema kuwa juhudi hizo zimeweza kuzaa matunda na kuweza kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya ugonjwa huo kutoka asilimia 80 miaka kumi iliyopita mpaka 20 kwa sasa.
Alisema kuwa wizara yake iliendesha kampeni ya ugawaji wa madawa kwa wanafunzi ikiwa pamoja na kuwapatia elimu ya usafi na tiba.
“Ni kwamba kwa sasa hali kidogo inaridhisha kwa kuwa tumeweza kukabiliana na tatizo hili la ugonjwa wa kichocho kwa kiasi kikubwa na leo huu msaada wa hawa wajerumani pia utatuwezesha kulimaliza tatizo hili kabisa” alisema kuwa Dk Sira.
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Merck Dr. Karl Ludwig Kley alisema kuwa kampuni yake imetoa vidonge milioni nne kwa ajili ya watoto na akina mama wa Pemba.
Alisema awali kampuni yake kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) inaendesha kampeni ya kupambana na ugonjwa huo Pemba mradi unaotarajiwa kuisha mwaka 2017.
Kampuni ya Merck ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali pamoja na madawa ya kukabiliana na ugonjwa wa kichocho kisiwani Pemba ambapo pia uongozi wa kampuni hiyo ulipata nafasi ya kutembelea Maabara ya Pemba inayokabiliana na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment