Michuzi Media Group ikishikiriana na Kampuni ya Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya www.issmichuzi.blogspot.com Kwa kupitia mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.
Akikaririwa na Ripota wetu katika mahojiano maalum,Mkurugenzi Mtendaji wa Michuzi Media Group,Ndugu Muhidin Issa Michuzi alisema, “Ni mapinduzi ya kweli ambapo Watanzania wataweza kuchukua hatua katika kuleta taarifa mbalimbali kwa wananchi kwa viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi (Libeneke la Globu ya Jamii) itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.
Nae Bwana Rajabu Katunda kutoka Uhuruone alisema kuwa , “Uhuruone imejikita katika kutoa huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa kuwafikia wanajamii kwa urahisi na kwa haraka. Tovuti nyingi zinatembelewa na Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii siyo haki.

Kwa pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini kwamba hili wazo litafuatwa na wengine.
Kwa msisitizo Bwana Michuzi aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”
Kutembelea tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au Laptop yako. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda moja kwa moja kwenye tovuti ya www.issamichuzi.blogspot.com.
Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo,issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze kuunganishwa.
No comments:
Post a Comment