HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 7, 2012

Dk. Shein afungua Mkutanom wa Mbegu Zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa Mbegu kwa nchi za Afrika ,( 12 AFSTA CONGRESS 2012) alipokuwa akiufungua mkutano huo leo katika ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort,nje ya kidogo ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(kulia)akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mauzo na Biashara,Injinia Maher El-Sayed M.Khalil, (Misr Hytech Seed Int. S.A.E) ,alipotembela maonesho ya mbegu za aina mbali mbali za mazao ya kilimo kutoka nchini Misri, alipofika kuufungua Mkutano wa siku tatu wa Mbegu kwa nchi za Afrika,(12 AFSTA CONGRESS 2012) katika ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji Unguja,(wapili kulia) ni Waziri wa Kilimo Serikali ya Muungano Prof Jumanne Magembe.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Shein,(katikati)akiangalia mbegu za aina mbali mbali za mpunga kutoka kampuni ya mbegu ya Vibha,Nchini India,katika maonesho ya biashara za mbegu,wakati wa mkutano wa siku tatu kuhusu mbegu kwa nchi za Afrika ulioanza leo katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji wa Unguja,(kutoka kulia) P Vidya Sagar,Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Vibha Seeds,Patrick Ngwediagi,Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya za Wafanya Biashara wa Mbegu wa Afrika (12 AFSTA CONGRESS 2012),na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Muungano Prof
Jumanne Magembe,(kushoto).
Baadhi ya wajumbe kutoka Nchi mbali mbali wa mkutano wa siku tatu kuhusu mbegu kwa Nchi za Afrika (12 AFSTA CONGRESS 2012),wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Shein,(hayupo pichani) akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ulioanza leo katika ukumbi wa Hotel ya Zanzibar beach Resort Nje ya Mji wa Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman IKULU ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad