HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 12, 2012

Ajali Mbaya yatokea Mkoani Dodoma njia panda ya Kiteto

Ajali mbaya sana imetokea jana majira ya saa tisa/kumi katika eneo la Mbande Mkoani Dodoma, Njia Panda ya kuelekea Kiteto ikihusisha magari matatu,likiwemo Lori aina ya Scania, Toyota Mark II na Toyota Carina ambayo ndio iliyoharibika vibaya san na kusababisha watu wawili wamepoteza maisha papo hapo.Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni gari hiyo aina ya Toyota Carina ilikuwa ikijaribu kuovertake Gari nyingine aina ya Toyota Mark II huku mbele kukiwa na hilo Lori aina ya Scania,hali iliyompelekea dereva gari hiyo aina ya Carina kushindwa kulipita lile gari lingine na kujikuta ikiigonga ile gari nyingine na kwenda kujipiga tena kwenye Lori hilo.Abiria waliokuwemo kwenye hiyo gari aina ya Toyota Carina ndio waliofariki papo hapo ambapo mmoja alikuwa ni mgonjwa na alikuwa akikimbizwa hospitali (kwa mujibu wa mtoa taarifa) huku deveva ambaye alionekana kuwa ni mzima aliwahishwa hospitali kwa matibabu ya haraka.
Hii ndio gari aina ya Toyota Mark II inavyoonekana baada ya kugongana na hiyo gari nyingine 
Mmoja wa wasamalia waliofika katika eneo la tukio akijaribu kuangalia kama anaweza kuwatambua Marehemu waliokuwemo kwenye gari hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad