HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 27, 2012

WASHILI WADAI HAWAPO TARARI KUKUTANA NA KIKUNDI AMBACHO KINAZALILISHA KABILA LAO

NA MERY AYO, ARUSHA

VIONGOZI wa Kimila wa kabila la Wameru, (WASHIRI)wamesema kuwa hawako tayari kuona mtu au kikundi chawatu kikitumika kuridhalilisha kabila hilo kwa mila na desturi zake kwa kisingizio cha kutafuta umaarufu wa kisiasa watazilinda mila na desturi zao kwa gharama yeyote ile.

Kauli hiyo imetolewa jana na Viongozi wa kabila hilo walipokuwa wakizungumza na wanahabari kuelezea taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari zikisema kuwa wazee hao wamekubali kutoa msamaha kwa mbune wa Arusha, na kumshangaa msajili wa vyama vyasiasa John Tendwa.

Akizungumza kwa niaba ya Washirii, wenzake nyumbani kwake Akheri, Mshiri mkuu Hezron Sumari, amesema kuwa wanashangaa habari hizo kuchapishwa kwenye vyombo vya habari wakati wao hawajaonana na viongozi hao na kueleza kuwa waliotoa habari hizo ni vikundi vya wahuni .

Wamesema kuwa wao hawajaotaka mtu kikundi au Chama kuwaomba msamaha wowote, kutokana na kitendo kilichofanywa na mbunge waArusha, Godbles Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki Jeremia Solomooni Sumari, ambapo mbunge huyo aliugeuza msiba jukwaa la kisiasa.

Alisema kitendo hicho kimewadharirisha na kuwafgedhehesha kwa sababu hawakutegemea mtu mwenye wadhifa wa ubunge angelifanya kitendo hicho na kutangaza habari za Chama chake wakati wao wako kwenye huzuni.

Alisema kuwa tayari Wameru, wamemtambua mbunge huyo kwa ni mtu wa vurugu, kwa kwao vurugu hazikubalriki na kamwe hazina nafasi na hivyo hawana nafasi ya kumpokea mtu wa aina hiyo katika jamii zao.

Alisema Washiiri, ni viongozi wa Mila na Desturi hivyo lazima wazilinde na kuzitetea kwa gharama yeyote ile hivyo hawako tayari kupokea msamaha wa mtu yeyote au kikundi au chama kwa sababu wamedharirika .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad