HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 13, 2012

WALEMAVU WAMWOMBA RAIS KUWAPATIA NAFASI TATU ZA WAWAKILISHI WA UUNDAJI WA KATIBA

Na Mery Ayo,Arusha

JAMII ya walemavu nchini wamaemwomba rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anawapatia nafasi tatu za wawakilishi wao katika mchakato mzima wa uundaji wa katiba mpya.

Ambapo jamii ya walemavu imekuwa ikisahulika katika nyadhifa mbali mbali jambo linalofanya jamii hiyo ikose wawakilishi wao wa kuwatetea katika maswala mbali mbali .

Hayo yalisemwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la walemavu linaloshughulkia haki za kisheria ,maendeleo ya jamii na uchumi bw Gideon Mandesi wakati akiongea na watoto walemavu kutoka mkoa wa arusha

Alisema kuwa endapo kutakuwa na wawakilishi wa walemavu katika mchakato mzima wa katiba mpya utarahisisha kwa kiasi kikubwa sana kuwa na watu wak kushughulikia kero zao amzimekuwa zikiwakabili siku hadi siku.

Aidha alifafanua kuwa kuwepo kwa wawakilishi pia kutasaidia kuwahamasisha walemavu kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao katika nmchakato wa katiba mpya na hatimaye kuweza kurekebishwa kwa sheria ya mwaka 2010 ambayo inawashughulikia wale wote wanaokikuka sheria ya walemavu.

Alieleza kuwa kupita na fasi hizo kutasaidia kwa kiasi kukubwa kuwasaidia walemavu kupata sehemu ya kuelezea kero zao na kuweza kutatuliwa kwa haraka.

Kwa upande wao watoto walemavu waliitaka jamii kwa ujumla kuacha kuwaita majina ya udhalilishaji kwa kuwa sii wao walipenda kuwa walemavu,kwani wengi wao wamekuwa wakiwatania kwa majina ambayo hayastahili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad