HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2012

TBL NA MWANAMUZIKI LADY JAY DEE WAANZA KUTUMIA BARCODES ZA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa TPSF,Godfrey Simbeye (kulia) akikabidhi Bango lenye alama za mistari (Barcodes) kwa Mkurugenzi wa Machozi Co. LTD, Gadner Habash wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa alama hizo za mistari iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Bidhaa Tanzania wa Wizara ya Viwanada na Masoko,Odilo Majengo (kulia) akikabidhi Bango lenye alama za mistari (Barcodes) kwa Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania, Steven Kilindo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa alama hizo za mistari iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya GS1 Tanzania,Fatuma Kange (kulia) akiwa katika picha na Gadner Habash (pili kushoto) pamoja na Mdau Pius Micky (kushoto) na baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya GS1 (TZ).
Picha ya Pamoja.

Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) imekuwa kampuni ya 127 kujiunga na mfumo wa alama za mistari yaani Barcodes za Tanzania,huku Mwanamuziki Judith Wambura Mbibo aka Lady Jay Dee akiwa ni msanii wa kwanza kutumia Barcodes za Tanzania kwenye albamu yake mpya inayojulikana kwa jina la The Best Of Lady Jay Jee ambao ni albamu yake ya 5.

Kwa kujiunga huko kunafanya jumla ya bidhaa zaidi ya 1800 ambazo ziko sokoni zinazotumia alama za mistari za Tanzania zinazotolewa na Kampuni ya GS1 (TZ) National Limited.

Awali kabla ya kujiunga na GS1 Tanzania, TBL walikuwa wakitumia alama za mistari toka GS1 South Afrika na hivyo bidhaa zao kuwa ana alama za mistari toka Afrika ya Kusini na Kenya.

Pia kwa upande wa wasanii hapo awali walikuwa wakilalamika kuhusu kuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji wa kazi zao kimasoko hivyo basi kwa kutumia Barcodes msanii kupitia meneja wake anaweza kupeleka kazi zake mwenyewe kwenye Supermarkets na kufuatilia mauzo bila kutumia mtu wa kati na hivyo kupunguza utegemezi wa wasambazaji wasio rasmi.

Kwa kumpatia Lady Jay Dee Barcodes tunadhani huu utakuwa mwanzo mzuri kwa kushirikiana na BASATA na vyombo mbali mbali vinavyosimamia kazi na haki za wasanii kutengeneza mfumo wa ufuatiliaji kazi hizi kwa kutumia mfumo wa ufuatiliaji wa GS1 (Traceability) ili kupata ufumbuzi.

Kampuni ya GS1 ambayo imeanzishwa kwa ushirikiano wa serikali na asasi za sekta binafsi ndiyo pekee yenye idhini ya kutoa alama hizo muhimu katika sekta ya uchumi na biashara nchini.

Awali makampuni ya Tanzania yalikuwa yakipata huduma hizi toka nchi jirani ya Kenya na Afrika Kusini.

Kutokuwa na alama za mistari Nchi ilikuwa ikipoteza takwimu nyingi za kibiashara kwani ili uweze kuuza bidhaa zilizokamilika (Finished Products) kwenye soko la kimataifa ni lazima uwe na alama za mistari, kwa kutumia alama za nchi nyingine Tanzania ilikuwa inaongeza Takwimu za nchi nyingine kwenye takwimu za uchumi duniani na hivyo kuonekana inauza kidogo nje.

GS1 Tanzania ina miezi sita tangu ianze huduma zake nchini Tanzania na tayari makampuni ya kizalendo 127 yameshajiandikisha na huduma hii ikiwemo moja toka Demokrasia ya Kongo.

Kuna changamoto nyingi ambazo kampuni hii imekuwa ikikut na nazo kubwa ikiwa uelewa wa mfumo mzima na umuhimu wake hivyo elimu zaidi inabidi itolewe kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wazalendo kuweza kujitokeza na kujiunga ili watumie alama hizi zinazotambulika na kukubalika kimataifa.

Changamoto nyingine ni kwa makampuni mengi makubwa kuendelea kutumia alama za mistari toka nchi za nje, GS1 imekuwa ikiendesha warsha mbali mbali na kuwatembelea wafanyabiashara na kuwaeleza umuhimu wa kutumia alama za mistari za Tanzania, Bado muitikio ni mdogo lakini tunaimani elimu imeanza kuwaingia na kwa makampuni makubwa kama TBL kurejea nyumbani kunaweza wavutia makampuni mengine kuja kutumia Barcodes za Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania Mkoa wa Dar Es Salaam ndio unaongoza kwa wafanyabiashara wengi kujiunga na kuchukua Barcodes wakifuatiwa na mikoa Kilimanjaro na Arusha huku mikoa mingine kama Ruvuma, Rukwa ikiwa na takwimu ndogo sana za wafanyabishara kujiunga na mfumo huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad