HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 29, 2012

MKURUGENZI PRECISION AIR AHIMIZA MICHEZO NA UTALII WA NDANI NCHINI

Wafanyakazi wa Precision Air walioshiriki katika mbio za Kili Marathon hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Patrick Ndekana akifurahia kumaliza mbio za Vodacom Fun Run.
Afisa Mawasiliano wa Precision Air Amani Nkurlu (wapili kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake kabla ya kuanza kwa Vodacom Fun Run.
Kaimu Mkurugenzi Patrick Ndekana akiwapongeza wafanyakazi wa Precision Air Isaac Kibuga (kushoto) na Faraji Komba (kulia) waliojishindia medali baada ya kumaliza mbio za kilomita 21.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Patrick Ndekana ametoa wito kwa watanzania kushiriki katika michezo na utalii wa ndani ili kuweza kushindana kimataifa na kujenga utamaduni wa kuenzi urithi wetu.

Akizungumza mkoani Moshi hivi karibuni kama mdhamini wa Kilimanjaro Marathon, Ndekana alisema, “Tanzania ina vipaji vingi sana katika michezo, ikiwemo riadha. Naamini kabisa kwamba wadau tukijipanga vizuri tutaweza kuibua majina makubwa wa michezo kutoka taifa hili.”

“Kwa kutambua umuhimu huu ndo maana sisi kama Precision Air tumeweza kudhamini riadha hizi kama wasafirishaji rasmi (Official Carriers) kama njia ya kusaidia na kuinua michezo nchini,” alisema Mkurugenzi huyo ambaye pia alishiriki katika mbio hizo.

“Ila lazima tuongeze munkari ya kujifunza, kukuza vipaji toka udogoni, na viongozi wa michezo wetu waweze kujitahidi kuwatafutia wachezaji wetu nafasi za kung’ara, huku sisi wadhamini pia tukitumia nafasi zetu kwa kuendelea kutoa sapoti,” alisema.

Kwa upande mwingine Ndekana alitoa pia wito kwa watanzania kujenga desturi ya kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro na mbuga mbali mbali za wanyama zilizopo nchini.

Akizungumzia umuhimu huo Bw Ndekana alisema, “Nchi yetu Tanzania ina vivutio na rasilimali nyingi sana, ikiwemo huu mlima maarufu….ingekuwa vizuri kwa sisi pamoja na watoto wetu na vizazi vijavyo kuja na kuweza kujifunza asili yetu kwa kutembelea haya maeno kuliko kuishia kuona tu katika luninga au kusoma katika vitabu.”

“Lakini pamoja na hayo hii itakuwa fursa nzuri pia kuchangia katika pato letu la taifa na kuzidi kuinua sekta yetu ya utalii nchini,” alisema Ndekana.

Bw. Ndekana pia aliwakaribisha umma kusafiri na shirika hilo la ndege kuweza kutembelea vivutio vya utalii mbali mbali nchini kwa sababu shirika hilo linasafiri karibu kila kona ya nchi ikiwemo sehemu kama Kilimanjaro, Mwanza, Zanzibar na kadhalika huku akisisitizia kuwaptia huduma bora kwa wasafiri wake.

Hii ni mara ya pili sasa kwa Precision Air kudhamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon yanayofanyika kila mwaka Moshi, Kilimajaro. Shirika hilo ina mtandao mkubwa nchini kuliko mashirika yote Tanzania, ikiwa inafanya safari kwenda; Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Kikanda Precision Air inasafiri kwenda Nairobi, Mombasa, Entebbe, Hahaya na Johannesburg.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad