Baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimuhudumia mmoja wa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wadi namba sita kwenye Jengo la Mwaisela kwenye hospitali hiyo.Madaktari hao ambao walikuwa kwenye mgomo kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo,leo wameanza tena kazi mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda jana na kuzungumza nae na kuafikiana kutekelezewa yale waliyoyahitaji.
Madaktari wa Muhimbili wakimfanyia matibabu mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo leo.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa wamekaa nje ya eneo ya huduma ya matibabu ya haraka wakisubiria wagonjwa wanaoletwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Wauguzi wa Muhimbili wakimtoa mgonjwa MOI na kupempeleka kwenye wadi iliopo kwenye jengo la Mwaisela.
Mgonjwa alipokelewa na wauguzi wa kitengo cha Huduma ya Haraka kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Pamoja na Kwamba Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamaliza Mgomo wao na kuanza kazi rasmi leo,wagonjwa wengi sasa hivi hawapo hospitalini hapo kama inayoonekana pichani.
Sehemu ya Kinamama wenye watoto wakiwa kwenye maeneo ya Hospitali hiyo na wamekuwa ni wenye furaha kwa kuona huduma zimerudi kama ilivyokuwa hapo awali hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment