HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 21, 2012

MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA BARABARA (RFB) NCHINI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UKARABATI WA MADARAJA NA MAKALAVATI YALIYOATHIRIWA NA MARURIKO JIJINI DAR

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa barabara (RFB) Dkt.James Wanyancha (kulia) akiongea na waandishi wa habari pichani hawapo baada ya kukagua eneo la daraja la Kibo- Msewe katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kaungalia matumizi ya maombi na mgao wa fedha za dharura kwaajili ya mkoa wa DSM zilizotolewa na mfuko wa Bodi ya Barabara kwajili ya kukarabati madaraja na makalavati yaliyoharibika na mafuriko mwaka jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Dkt, James Wanyancha (mbele) akifuatiwa na Mhandisi wa manispaa ya Kinondoni Gerald Urio pamoja na watendaji wengine wakikagua eneo la daraja la Kimara- Stop Over jijini Dsm , Mwenyekiti huyo amefanya ziara ili kukagua na kuangalia matumizi ya fedha za maombi na mgao wa fedha za dharura kwaajili ya mkoa Dsm zilizotolewa na RFB zaidi ya bilioni5 kwajili ya ukarabati wa madaraja na makalivati
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ya Delmonte ya Tanzania wakiwa kazini kukarabati daraja lililoharibiwa na mafuriko ya mwaka jana katika eneo la Kimara Msewe wilaya ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) Dkt, James Wanyancha (hayupo pichani) alikagua ili kuangalia matumizi ya maombi na mgao wa fedha za dharura kwaajili ya mkoa wa Dar es Salaam zilizotolewa ma mfuko wake zaidi ya shilingi bilioni tano (5,282,420,313)kwaajili ya dharura ya matengenezo katika mkoa huo.
Ukarabati ukiendelea kwenye eneo la draja la Kimara _Baruti Wilaya Kinondoni ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa RFB Dkt, James Wanyancha (pichani hayupo) alikagua maendeleo ya ukarabati.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad