Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni (Mstaafu),Chiku Gallawa akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Konstebo Henry Nyang'ombe askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani Tanga (FFU) aliyefariki na mwenzake Koplo Jeggy Kangaga wakati wakiwa katika msafara wa Makamu wa Rais, Dkt Mohamed Gharibu Bilal alipokuwa na ziara ya siku nne mkoani Tanga, Mwenye kanzu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tanga Bw. Mussa Shekimweri.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,SACP Constatine Masawe akitoa taarifa ya ajali kwa waombolezaji waliofika katika kambi ya kikosi hicho cha FFU kilichopo eneo la Majani Mapana Jijini Tanga. wengine waliokaa kwenye viti kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Dkt Ibrahim Msengi, Mkuu wa wilaya ya Lushoto Sophia Mjema na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima.
Askari G1752 Konstebo Henry Nyang'ombe (25) ambaye alijiunga na jeshi hilo mwaka 2008 alisafirishwa kwenda kijijini kwao Makongoro kilichopo kata ya Buturi wilayani Mara kwa mazishi.
Askari E 1192 Koplo Jaggy Kangaga (43) ambaye alijiunga na jeshi hilo mwaka 1987 kabla ya mwaka 2008 kupandishwa cheo na kuwa Koplo alichokuwa nacho hadi mauti yalipomkuta, alisafirishwa kupelekwa kijijini kwao Mwakisandu kilichopo wilayani Meatu mpakini mwa Maswa.
sehemu za waombolezaji wakiwemo askari wa kikosi cha polisi cha FFU wakiwa na hudhuni kuondokewa na wenzao hao, wakifuatilia kwa makini taarifa mbalimbali zilizokuwa zikisomwa katika msiba huo.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw. Erasto Sima akijaribu kuwabembeleza ndugu za marehemu mara baada ya kutoka kutoa heshima zao za mwisho kisha kulipuka kwa kilio kutokana na huzuni za kuondokewa na ndugu zao hao. Kulia kabisa ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zipora Pangani.Picha na Mashaka Mhando, Tanga
No comments:
Post a Comment