Mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kila siku ya jumapili saa moja na nusu jioni katika kituo cha Televisheni cha Chanel Ten na aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu, wiki hii amekutana na baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers) na kufanya nao mahojiano wakizungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na mitandao ya kijamii na umuhimu wake katika jamii.
Kama anavyoonekana katika picha akiongoza kipindi hicho ambacho pia hurudiwa siku ya jumamosi na siku ya Jumatatu saa saba mchana, Hoyce Temu anauliza maswali mengi ambayo yanajibiwa na mablogger hao na kufafanua zaidi kuhusiana na mitandao hiyo.
Wadau wa mitandao ya kijamii mnaweza kufuatilia mahojiano hayo kupitia luninga zenu katika kituo cha televisheni cha Chanel Ten hiyo leo jioni ili kujua yapi yalizungumzwa katika mahojiano hayo.
Mmiliki wa http://fullshangwe.blogspot.com/ Bw. John Bukuku akifafanua jambo katika mahojiano hayo.
Mmiliki wa http://8020fashions.blogspot.com/ Shamimu Mwasha akielezea changamoto anazokumbana nazo kama mwanamke katika kazi yake kama Blogger hapa nchini.
Mmiliki wa http://www.mjengwablog.com/ Bw. Maggid Mjengwa kutoka Iringa akichangia mada katika mahojiano hayo yaliyofanyika katikati ya wiki hii jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment