Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB),Noves Moses (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni mchango wa Benki hiyo kuisaidia shule ya msingi Temeke ambayo mbali na kuwa na wanafunzi wa kawaida pia inakitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia ( Viziwi). kukabiliana na changamoto zake mbalimbali.Kulia kwake ni meneja wa kitengo cha mikopo benki ya posta Abdallah Mtandika,Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya msingi Temeke,Rajab Ndunda na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Temeke Bakir Makele.
Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses (kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa Mkuu wa shule ya msingi Temeke,Said Mbolembole (kushoto). Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo. Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya shule Rajab Ndunda na Meneja wa kitengo cha mikopo benki ya Posta Abdallah Mtandika.
Meneja wa kitengo cha mikopo benki ya Posta Tanzania Abdallah Mtandika akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa wadau mbalimbali kuchangia elimu ya watoto wetu kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 2 kwa shule ya Msingi Temeke.Kulia ni Meneja Uhusiano wa Benki ya Posta Noves Moses na mwenyekiti wa kamati ya shule Rajab Ndunda,kushoto ni mkuu wa shule hiyo Said Mbolembole.
No comments:
Post a Comment