HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 21, 2011

Msiba kwa kampuni ya InterGrated jijini Dar

Dj Machachari aliekuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya InterGrated Communications LTD,Amos Dotto amefariki Dunia leo asubuhi wakati akiwa safarini mkoani Tabora kuelekea nyumbani kwao Ushi Rombo mkoani Shinyanga.

Marehemu Amosi amefikwa na mauti hayo kutokana na Maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu,Kwa sasa mipango ya mazishi inapangwa kwa ushirikiano wa ndugu,jamaa,marafiki na wafanyakazi wenzake wa kampuni hiyo ya InterGrated.

Amosi katika uhai wake alikuwa Dj maarufu wa vipindi mbalimbali katika vituo vya runinga.Aidha alikuwa Dj maarufu wa Kampuni hiyo ya Integrated hasa kwenye promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na kampuni hiyo.

Kupitia Globu ya Jamii tunaomba kuwafahamisha wanajamii na hasa wanataaluma ya habari na Djs wote kuhusu msiba huu mkubwa

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa,Jina la Bwana Lihimidiwe.

Amein.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad