Mkuu Mkoa wa Rukwa Mhandisi,Stella Martin Manyanya (MB)akizindua rasmi mradi wa umeme unaotumia nishati ya upepo katika Chuo cha Ualimu Rukwa (Rukwa Teachers Collage) kilichopo katika kijiji cha kanondo Katika manispaa ya Sumbawanga. Mradi huo wa Umeme umebuniwa na mjasiriamali kutoka Rukwa wa Kampuni ya Ulaya Hydro and Windmill Technology. Mradi huu wa umeme utatumika katika chuo hicho cha ualimu kwa shughuli mbalimbali ikiwemo chumba cha kompyuta, mabwenini na madarasani. Mkuu huyo wa Mkoa alifarijika na kutoa ushauri kwa wajasiriamali kuonyesha uwezo wao kwa kubuni miradi mbalimbali ambayo ina manufaa ya moja kwa moja kwa jamii.
Mkoa wa Rukwa Mhandisi , Stella Manyanya akionesha hadharani tuzo ilichopewa asasi ya kijamii iitwato Rukwa Women Advancement Association (RWAA) iliyoko mjini Sumbawanga katika mahafali ya kwanza ya waalimu wa awali hafla iliyofanyika katika Chuo cha Ualimu cha Rukwa , tuzo hiyo ilitolewa na the Foundation for Civil Society mwaka hu kwa kutambua mchango wa asasi hiyo kwa jamii , RWAA imeanzisha na kumiliki Chuo cha Ualimu na Chuo cha wauguzi vyote vipo kijijini Kanondo , Mkuu huyo wa Mkoa aliguswa na maendeleo ya taaasi hiyo na kusema kuwa ni mfano wa kuigwa na kuwaasa wanawake wengine kuwa na umoja kwa kujijenga kijasiriamali na kuwekeza katika miradi inayotoa faida kwao na jamii kwa ujumla.
Kikundi cha sanaa cha Kanondo kutoka Wilayani Sumbawanga kikweaburudisha katika mahafali ya kwanza ya waalimu wa awali iliyofanyika jana katika Chuo cha Ualimu kilichopo katika kijiji cha kanondo katika Manispaa ya Summbawanga (Picha na Peti Siyame).

No comments:
Post a Comment