Mtaalam wa Kilimo toka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) ,Dkt. Delphina
Mamiro akitoa mafunzo ya kilimo kwa Kina Mama wanaoshiriki Shindano la
Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa na Shirika la Oxfam.Kina Mama hao
ambao wameingia katika hatua ya kumi bora wapo kwenye kambi iliopo
kwenye hoteli ya Rombo Green View,Sinza jijini Dar es Salaam.Mshindi
katika Shindano hili atapata Trekta mpya atakalolitumia kwa kazi zake za
kilimo.
Mwakilishi wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ambaye pia ni jaji wa
Shindano hilo,Bi. Joyce Mvuna akiwafafanulia jambo washiriki wa
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula,wakati semina ya Mafunzo ya Kilimo
Bora inayoendelea kufanyika katika Hoteli ya Rombo Green View,Sinza
jijini Dar es Salaam.Mshindi wa Shindano hili la Mama Shujaa wa Chakula
atapata Trekta atakalolitumia katika kilimo.
Mmoja wa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula,Bi. Anna
Olushuro akichangia mada wakati wa semina ya mafunzo ya kilimo bora
yanayoendelea katika kambi yao iliyopo katika hoteli ya Rombo Green
View, Sinza jijini Dar es Salaam.
Moja ya Kundi la Kina Mama walioingia katika hatua ya Kumi bora ya
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula,wakijadiliana jambo ambalo
wataliwasilisha kwa makundi mengine na kuchangia mada kwa ujumla.kutoka
kushoto ni Ruzena Binamu (Lind),Anna Olushuro (Morogoro),Getrude Anthony
(Kagera) na Mwandiwe Makame (Kaskazini Unguja).
No comments:
Post a Comment