wafanya biashara wadogo(machinga) wakifanya biashara karibu kabisa na mitambo ya kusambaza umeme Ubungo
Mdau Raymond Mkandawile ametuletea hii wakati akiwa katika maeneo ya Ubungo Jijini Dar,amejionea hali isiyo ya usalama katika maeneo hayo ambapo wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga wamekuwa wakifanya biashara katika mazingira hatarishi sana hasa ukizingatia kuwa eneo hilo limezungukwa na mitambo ya kuzalisha na kusambaza umeme jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha ya wafanya biashara hao,lakini pia waendao kwa miguu na wanunuzi.
Hatari hiyo inatokana na ukweli kwamba watu huwa wengi jioni katika eneo hilo jambo linaweza kusababisha maafa makubwa sana iwapo janga la moto litatokea katika eneo hilo.
Daima kinga ni bora kuliko tiba hivyo ni ombi letu kwa serikali kuliangalia jambo hili kwa upana zaidi ikiwa ni pamoja na kupitia alama za kiusalama ili kuepusha janga lolote kutokea katika eneo hilo badala ya kusubiri janga kutokea ndipo ikumbukwe kuunda tume ya kuchunguza wakati tayari maisha ya watu wasio na hatia yatakuwa yamepotea.
No comments:
Post a Comment