Wahariri wa vyombo vya habari nchini,wakitembelea kiwanda cha bia cha TBL,wakati wa ziara yao. `
Mtaalamu wa Mafunzo ya Utengenezaji bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Rose Mrina (wa pili kulia), akimuelezea Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya magazeti ya New Habari, Deodatus Balile jinsi kiwanda cha bia kinavyofanyakazi, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la The Guardian, Wales Maugo na Mnaku Mbani ambaye ni Mhariri wa gazeti la Business Times.
Meneja Uhusiano wa TBL, Edith Mushi akiwashukuru wahariri kwa kukubali mwaliko wa kutembelea TBL.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kulia), akibadilishana mawazo na Mhariri gazeti la The East African, Joseph Mwamunyange (katikati), pamoja na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Deodatus Balile baada ya kufanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari, katika Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam, ambapo aliwaeleza kuhusu utendaji na mafanikio ya kampuni hiyo.
Mtaalamu wa Mafunzo ya Utengenezaji bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Rose Mrina, akiwaelezea wahariri kuhusu zao la shayiri linalotumika kutengenezea bia.
Wahariri wakiwa chumba cha kompyuta zinazotumika kupikia bia katika kiwanda cha TBL
Meneja Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia), akielezea mbele ya wahariri wa vyombo vya habari,kuhusu jinsi TBL ilivyoweka kipaumbele chao kusaidia jamii katika miradi ya maji nchini. Wahariri walialikwa kutembelea kiwanda cha bia kilichopo Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment