Mkuu wa Wilaya ya Rorya Bw. Benedict Kitenga (kulia) akaikata utepe kufungua madarasa mawili yaliyojengwa katika shule ya Sekondari ya TAI wilayani Rorya kwa msaada wa Vodacom Foundation yenye thamani ya shilingi milioni 30, (kushoto) ni Meneja wa mfuko wa huduma za kijamii (Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule.
Meneja wa mfuko wa huduma za kijamii wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule (kulia) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya TAI iliyoko Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, (kushoto) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Richard Okore.
Haya ndiyo madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa na mfuko wa huduma za kijamii (Vodacom Foundation) katika Shule ya Sekondari ya TAI iliyopo Rorya Mkoani Mara ikiwa ni sehemu ya shuguli za mfuko huo kwa jamii.
No comments:
Post a Comment