KUNDI
jipya la taarab linalokuja kwa kasi nchini, Tanzania Modern Taarab
(T-Moto) ama ‘Real Madrid’ linatarajia kuanza kufanya maonyesho mawili
katika mkoa wa mtwara.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa mara
tu baada ya uzinduzi wa kundi hilo unaotarajia kufanyika Oktoba 28,
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, kundi hilo tayari
linamwaliko wa Oktoba 29 na 30, Mkoani Mtwara.
Aidha
alisema kuwa mara tu baada ya kumaliza onyesho la uzinduzi huo, wasanii
wataondoka jijini usiku huo huo kuanza safari ya kuelekea Mtwara ambako
watafanya maonyesho mawili.
Onyesho
la kwanza la oktoba 29, linatarajia kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli
ya Makonde Beach Club, na onyesho la pili litafanyika Oktoba 30
Nachingwea.
Pia
Salmini alisema kuwa kabla ya kufanya onyesho la pili wasanii wa kundi
hilo watatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa huo husasan wodi ya
wazazi na watoto, ambapo watatoa msaada wa kitanda cha kuzalia cha
wajawazito katika hospitali hiyo pamoja na kutoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa watoto waliolazwa katika hospitali hiyo.
Aidha
katika uzinduzi wa kundi hilo unaotarajia kufanyika katika Ukumbi wa
Diamond Jubilee, Bendi za Mapacha Watatu na Msondo Ngoma, zitakuwa bega
kwa bega katika kutoa burudani za kusindikiza na ‘kusapoti’ kundi hilo.
“Tayari
maandalizi yote ya uzinduzi yamekamilika ikiwa ni pamoja na mazoezi ya
kutosha wanayoendelea nayo wasanii wa kundi letu ambao hadi sasa wapo
Kambini wakitarajia kuvunja kambi siku moja kabla ya uzinduzi” alisema
Amini
Albam
hiyo ya kwanza ya kundi hilo imebebwa na wimbo wa Bi Mwanahawa Ally,
uitwao Aliyeniumba Hajanikosea, ambapo pia itakuwa na nyimbo nyingine
kali zilizoanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio.
Nyimbo
nyingine ni wimbo wa Jokha Kassim, ambao tayari umeshaanza kuzua gumzo
miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Taarab, ambao hauishi kujadiliwa,
uitwao Unavyojidhani Hufanani.
Nyingine
zinazokamilisha albam hiyo ni pamoja na Mchimba Kaburi Sasa Zamu yake
Imefkuwa ni ‘Dongika, ulioimbwa na Mrisho Rajab, aliyejitosa katika fani
ya muziki wa Taarab akitokea katika shindano la BSS, pamoja na Riziki
Shotcut, ulioimbwa na Aisha Masanja.
No comments:
Post a Comment