Bingwa Mpya wa UBO katika uzito wa Bantum,Francis Miyeyusho akifurahia ubingwa wake huo wakati akivishwa mkanda wake na Mlezi wa Mchezo wa Ngumi hapa nchini,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Afande Suleiman Kova na Diwani wa Kinondoni,Mh. Abbas Tarimba,huku mpinzani wake,Mbwana Matumla (shoto) akiwa amejawa na huzuni kwa kuupoteza ubingwa huo.Francis Miyeyusho kanyakuwa ubingwa huo baada ya kumchakaza vibaya Bingwa wa Zamani UBO,Mbwana Matumla katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall.
Bondia Francis Miyeyusho ampatia konde kali sana mpinzani wake,Mbwana Matumla wakati wa mchezo wao uliomalizika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall.Francis Miyeyusho kanyakua ubingwa katika mchezo huo kwa kushinda Mbwana Matumla kwa point.
Hapa ilikuwa ni piga nikupige.
chukua hiyoooo.....,holaaaaa.. kiukweli mpambano huu ulikuwa ni mkali sana na wakusisimua.
Ni wakati wa Miyeyusho sasa kung'aa kwenye ngumi.Hongera Francis
ReplyDelete