Bryan Robson mchezaji wa zamani wa Mancester United (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wacheza ngoma za asili nchini Tanzania wa kundi la Afrikanasha
wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya soka ya U-17 Airtel Rising stars
inayoshirikisha vijana toka Kenya, Malawi, Siera Leone, na Tanzania
inayoanza leo jumapili


Mwanasoka Nguli wa Klabu kongwe ya Manchester United Bryan
Robson akipiga mpira mara baaada ya mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani
leo kuashiria uzinduzi rasmi wa Clinic ya soka kwa vijana wa U-17 ujulikanayo
kama Airtel Rising Stars itakayoanza rasmi nchini Tanzania kuanzia wiki
ijayo tarehe 30 octobar kwa lengo la kusaidia kukuza vipaji vya vijana nchini
Tanzania, Malawi Kenya na Siera Leone. Uzinduzi wa clinic ya Airtel Rising
Stars ulifanyika katika hoteli ya Sea Cliff Jijini Dar es salaam
·
Mpango kabambe
wa Airtel Rising Stars utakaojumuisha vijana 11,000 kutoka nchi 15 barani
Afrika kuzinduliwa julai mwakani
·
Airtel
kushirikiana na mashirikisho ya soka kusaka vipaji na kuviendeleza
·
Wachezaji
kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Malawi na Sierra Leone wanashiriki
kliniki ya soka nchini Tanzania chini ya mpango wa shule za Manchester United
Mchezaji nguli wa
Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Bryan Robson amezindua rasmi
kliniki ya siku nne ya kimataifa ya Airtel Rising Stars inayofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia Jumapili Oktoba 30 na kumalizika
Alhamisi Novemba 3, 2011.
Kliniki
hiyo ambayo inajumuisha washiriki kutoka nchi za Kenya, Malawi, Sierra Leone na
wenyeji Tanzania ina lengo la kukuza vipaji vya soka vya vijana hao
waliopatikana wakati wa mashindano ya Airtel Rising Stars katika nchi zao na
kujumuisha wanafunzi wa shule za sekondari wenye umri chini ya miaka 17.
Ikiwa
mwenyeji, Tanzania imepata fursa pekee ya kushirikisha wachezaji sita wakati
Kenya imeleta washiriki wanne, Malawi na Sierra Leone zinawakilishwa na
wachezaji wawili kila moja. Wachezaji kutoka Tanzania ni Dennis Richard,
Seleman Mbovu, Samir Omar, Charles John, Graham Naftali na Kassim Jungu. Kutoka
Kenya ni Naim Ashraf, Mzee Ali Rama, Naomi Njeri na Emily Auma. Washiriki
kutoka Sierra Leone ni Patrick Gbinda na Hamza Kamarana kutoka Malawi ni Amidu
Mapila na Chimwemwe Billy.
Mpango wa soka kwa vijana wa Airtel Rising Stars ulizinduliwa
mwezi Julai kwa kushirikiana na moja ya timu kubwa duniani, Manchester United. Mpango huu unafanyika kuanzia katija ngazi ya mkoa na taifa na
kuhitimishwa kwa kliniki za aina yake nchini Gabon na Tanzania chini makocha
kutoka Manchester United.
Ufunguzi wa kliniki inayofanyika Dar es Salaam ulifanywa na
mchezaji mahiri wa kiungo wa Manchester United Bryan Robson. Kapteni mstaafu wa
timu ya Taifa ya Uingerza, Robson aliichezea Manchester United kwa mafanikio
kwa misimu 10 alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo aliyotwaa mataji
mawili ya ligi kuu na matatu ya FA kuanzia msimu wa mwaka 1981-1982 hadi
1993-1994.
“Nina furaha
kwamba mpango wa Airtel Rising Stars una lengo la kuwafaidisha wachezaji
chipukizi wenye umri chini ya miaka 17, ambao kwa maoni yangu, ndiyo nguzo
kubwa ya mafanikio ya mpira wa miguu”, alisema mchezaji huyo mstaafu wa
Uingereza na kupongeza kampuni ya Airtel kwa kubuni na kuanzisha mpango huu
aliouelezea kuwa muhimu kwa maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu barani
Afrika.
Alisisitiza kuwa njia ya kuelekea kwa mafanikio ya kweli ya mpira
wa miguu lazima ianze kwa kutilia mkazo programu za vijana kama mpango huu wa
Airtel unavyofanya. “Mimi mwenyewe niliweza kufanikiwa katika soka kwa
sababu nilianza kucheza soka nikiwa mdogo”, alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Cheikh
Sarr alisema kwamba Airtel inajivunia kuwa sehemu ya programu hii yenye lengo
la kurahisisha upatikanaji wa vipaji vya soka. “Sehemu hii ya Airtel
Rising Stars pengine ni muhimu sana katika mashindano. Kambi hii itawapa vijana
fursa ya kukuza ujuzi wao na kuwafanya kuwa wachezaji wazuri.” Alisema
Sarr.
Aliipongeza Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na wadau wengine kwa kuikumbatia
programu hii ya soka ya Airtel na kuahidi kwamba Airtel itahakikisha mikoa
zaidi inashirikishwa mwaka ujao.
Akizungumzia kliniki hii, Mtendaji Mkuu wa Manchester United Bw.
David Gill alisema; “Kliniki ya soka ya Airtel Rising stars inawapa
vijana walioteuliwa kushiriki mazingira bora ya kujifunza chini mpango wa
mashule wa Manchester United wenye lengo la kuzalisha wachezaji wazuri wanoweza
kucheza mpira wa kuvutia”.
Aliongeza ya kuwa kliniki hizi zinafanywa kulingana na program za
Manchester United lakini zinafanywa kwa namna ambayo inawawezesha wachezaji
chipukizi ‘kujifunza kucheza kama vile ambavyo Manchester United
wanacheza’
Mbali
ya Airtel na Manchester United, AON, kampuni kubwa ya bima duniani vilevile
imejitokeza kudhamini kliniki hii pamoja na michuano ya Airtel Rising Stars na
itakuwa inatoa bima kwa washiriki.
Kliniki
hii inahitimisha mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka 2011. Programu hiyo
ilizinduliwa Juni mwaka huu na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United,
Andrew Cole aliyeicheaea klabu ya Manchester United kwa misimu saba na
kuisaidia kutwaa mataji matano kati ya 19 ya Ligu Kuu ya soka ya Uingereza
iliyojinyakulia hadi sasa.
Programu
ya Airtel Rising Stars ni mpango wa Afrika nzima wenye lengo la kuwajengea
mawakala, makocha, mamlaka za soka na wadau wengine fursa ya kuona vipaji vya
wanasoka chipukizi na kutumia fursa hiyo kuviendeleza ili kupata wachezaji
wazuri kwa faida ya taifa hapo baadaye.
No comments:
Post a Comment