Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel
Tanzania, Sam Elangallor akionyesha mtaala utakaotumika kwenye mafunzo ya maafisa
masoko na mauzo wa kampuni hiyo ili kujitengenezea utaalam zaidi wa kutoa
huduma bora kwa wateja wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya maofisa
masoko na mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa yote tanzania mafunzo hayo
yanayojulikana kama Airtel Centum Sales University
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel
Tanzania, Sam Elangallor akimkabidhi kabrasha Meneja Mauzo wa kanda Pwani
Bw Godfrey Kavishe wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya maofisa masoko na
mauzo wa kampuni ya Airtel wa mikoa
Airtel Tanzania kampuni ya simu za mkononi iliyoonea na
inayoongooza kwa kutoa huduma za gharama nafuu nchini. Leo imezindua
mpango mpya wa kuwaongezea ujuzi wafanyakazi wake kuhakikisha wateja wa Airtel
wanapata huduma bora zaidi.
Mafunzo haya ni muongozo kwa ajili ya timu za mauzo na
usambazaji, akiongea katika uzinduzi huo mkurugenzi mkuu wa Airtel bwana Sam
Elangalloor alisema, “leo tunazindua rasmi Chuo cha mauzo nchini Tanzania,
ambacho kimeundwa kwa mtazamo mahiri ili kutatua matatizo na kujibu maswali
mengi ambayo wafanyakazi wetu wamekuwa wakikabiliana nayo katika shughuli zao
za kila siku kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kila siku.
Tunadhamini wafanyakazi wetu
ambao ni rasilimali yetu kubwa kuliko zote na ndio maana tumeelekeza jitihada
zetu kwenye kuongeza ujuzi na ndio maana tumeunda mafunzo haya kuongeza kiwango
cha ufanisi na utoaji Huduma za hali ya juu kwa watanzania wote pande
zote za nchi hii .
Nchini Tanzania tayari mafunzo hayo yameshaanza kwa
kushirkisha jumla ya wanaofanyakazi 55 toka
kitengo cha kuhudumia wateja kwa kusambaza bidhaa na Huduma kwa wateja kutoka
mikoa yote.
(Airtel Centum Sales University) ni maendeleo ndani ya
“Ujuzi Mahiri”. Chuo hiki kinatilia mkazo shughuli mbalimbali hasa katika
vitengo vya mauzi na usambazaji kuhakikisha kile kilichofundishwa kinafanyiwa
kazi katika shughuli za kila siku. Mafunzo haya yatachukua muda wa miaka miwili
na nusu na yatakuwa na ngazi tano kuanzia uuzaji mpaka ngazi ya juu kabisa ya
ushindi.
No comments:
Post a Comment