
Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi,Mh Shamsi Vuai Nahodha akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni maalumu ya kuielimisha jamii,itakayojulikana kama "Unywaji wa Pombe Kistaarabu",uliofanyika kwenye hoteli ya Movenpick,jijini Dar,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Serengeti Breweries (SBL),Bwa.Richard Wells.Kampeni hiyo itatangazwa katika vyombo vyote vya habari ikiwa ni pamoja na Redio, Magazeti, Televisheni, na Mitandao, zikiwemo Blogs.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mh Shamsi Vuai Nahodha akipokea vifaa maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti SBL Richard Wells, vifaa hivyo vitakavyotumika nchini kote ili kuwapima madereva wanaoendesha magari wakiwa wamelewa.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga akionyesha baadhi ya vifaa vitakavyotumika kuwapima madereva kiasi cha ulevi wakati wakiendesha magari barabarani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh Nahodha akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na na kampeni hiyo ya Unywaji wa Pomebe Kistaarabu.Mh Nahodha amesema kuwa takwimu zinaonyesha mwaka 2007 ajali zilizotokea ni 17.617 huku vifo vikifikia 2838 wakati hasara ya mali ilikuwa ni shilingi Bilioni 508, ambapo makosa ya kibinadamu yaliyosababisha ajali yalikuwa asilimia 176.40%,Aidha Mh Nahodha ameishukuru kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL) kwa kuanzisha kampeni hiyo,ambayo amesema kuwa itasaidia sana kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, Majeruhi na Hasara ya mali nyingi zaidi kwa wanajamii..
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Richard Wells akizungumza katika uzinduzi huo mapema leo asubuhi.
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga akizungumza mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya serengeti (SBL) Bw. Ephraim Mafuru akifafanua zaidi kuhusiana na kampeni yao walioizindua leo,jijini Dar.
Mkurugenzi wa Mawasiliano/Mahusiano wa kampuni ya Serengeti Breweries (SBL),Teddy Mapunda akifafanua jambo kuhusiana na kampeni yao walioizindua mapema leo ya Unywaji pombe kistaarabu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) ambapo pia walishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo itakayoanza kutangazwa nchini kote hivi karibuni kwa njia mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Richard Wells akijadiliana jambo na Wazri wa Mambo ya Ndani nya Nchi,Mh Vuai Nahodha.
Pichani ni baadhi ya Wana habari na wageni waalikwa mbalimbali waliofika mapema leo kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya Unywaji pombe kistaarabu.
No comments:
Post a Comment