HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 5, 2011

WAZIRI CHAMI AZINDUA BODI YA VIPIMO

Baadhi ya wajumbe wa Bodi mpya ya Wakala wa Vipimo (WMA), wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Cyril Chami (wa tatu kulia), baada ya kuzinduliwa mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mjumbe, Paskali Massawe ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa EWURA, Mwenyekiti wa zamanni wa bodi hiyo ambaye ameteuliwa kuwa mjumbe, Hosea Kiula, Mwenyekiti mpya wa Bodi, Rose Lupembe na kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joyce Mapunjo.
Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Pascal Massawe ambaye ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Vipimo (WMA), akijitambulisha wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo, uliofanyika mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam. Mwenyekiti aliyemaliza muda wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), Hosea Kiula ambaye pia kateuliwa kuwa mjumbe wa bodi hiyo.
Waziri Viwanda,Biashara na Masoko, Cyril Chami (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake, Hosea Kiula. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa Bodi, Rose Lugembe.
Mkurugenzi wa Fedha na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Pascal Massawe (kushoto) ambaye ni Mjumbe mpya wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA),akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa WMA, Magdalena Chuwa baada ya hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo kumalizika, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad