Mtendaji wa Mtaa wa Kiungani Kata ya Kurasini Manispaa ya temeke,Theophilda Christopher akitoa maoni yake wakati wa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo watendaji wa Mitaa na Kata juu ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria chini Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara(TLS).
Wakili kutoka Chama cha wanasheria Tanzania Bara (TLS),Steven Madulu akitoa somo kwa watendaji wa Mitaa na Kata juu ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wenye shida mbalimbali na hawawezi kumudu gharama ya kuajiri wakili. Watendaji hao wanatoka wilaya za Temeke na Kinondoni.
Wakili kutoka Chama cha wanasheria Tanzania Bara (TLS),John Seka akiwafundisha watendaji wa Mitaa na Kata juu ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi wenye shida mbalimbali na hawawezi kumudu gharama ya kuajiri wakili. Watendaji hao wanatoka wilaya za Temeke na Kinondoni.
Baadhi ya Watendaji Mtaa na Kata kutoka wilaya za Kinondoni na Temeke mkoani Dar es salaam wakisikiliza kwa makini mafunzo ya kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi kwenye maeneo yao. Mafunzo hayo yanaendesha na Mradi wa Maboresho wa Sekta ya Sheria chini ya Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara(TLS).Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment