HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 19, 2011

TMK wanaume watinga ubalozi wa Tanzania - UK

Mh Naibu balozi akiwa, maofisa wa ubalozi katika picha ya pamoja TMK pamoja na promota wao George.

Salam,


URBAN PULSE CREATIVE na Miss Jestina Blog wanakuletea Ziara ya Wanaume kutoka kundi la  TMK wakiwalishwa na Mh Temba na Chege walipopata fursa ya kutembelea Ubalozi wetu hapa mjini London kabla ya kumaliza show zao hapa nchini Uingereza siku chache zilizopita. Vilevile waliweza  kutembelea idara mbalimbali na kujionea jinsi gani Ubalozi wetu hapa London unavyofanya kazi hususani  katika idara nyeti ya Uhamiaji inayoongozwa na ofisa Ambokile na Kupiga Picha za pamoja wakiwa na  Mh Naibu Balozi Mh Chabaka Kilumanga Pamoja  na baadhi ya maofisa wa Ubalozi.


Baada ya Ziara yao Freddy Mtoi Kutoka BBC alifanya nao mahojiano maalum  ndani ya ubalozi na yatarushwa hewani  duniani kote.


Asanteni,


 Ziara hii iliandaliwa na Urban Pulse pamoja na miss Jestina Blog Ikishirikiana na Ubalozi wetu
 Chege akitoa Changamoto
MH Naibu Balozi Chabaka Kilumanga kwenye picha ya pamoja TMK na Goerge Ubalozini
Promota wa TMK Goerge Stanley Kutoka Gonex Service Limited akiwa na Joel Chacha katika ubalozi wetu London
Chege na Temba wakiwa na ofisa wetu Ambokile katika ofisi ya uhamiaji
Freddy Mtoi kutoka BBC akianza mahojiano na Mh Temba wakati Chege anakusanya data

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad