HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 20, 2011

TBL YACHANGIA SH. MIL 10 KWA WAATHIRIKA WA AJALI YA MELI ZANZIBAR


Meneja Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo akikabidhi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi hundi ya Sh.milioni 10 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya kusaidia waathirika wa ajali ya Meli ya Mv.Spice Islander hivi karibuni.
Maofisa wa kampuni ya bia Tanzania wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi baada ya kukabidhi mchango wa sh. mil. 10 za kusaidia waathirika wa ajali ya meli ya MV. Spice Islander, mjini Unguja, Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Meneja Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia), baada ya kupokea mchango wa TBL, wa sh. mil. 10 za kusaidia waathirika wa ajali ya Meli ya Mv.Spice Islander iliyotokea visiwani Zanzibar hivi karibuni.  (Wa pili kulia ni Mwakilishi wa TBL, Zanzibar, Mweidady Mbaga na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Dorris Malulu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Zanzibar, Mweidady Mbaga baada ya kupokea mchango wa TBL, wa sh. mil. 10 za kusaidia waathirika wa ajali ya Meli ya Mv.Spice Islander iliyotokea hivi karibuni. Kulia ni Meneja Miradi Maalum wa kampuni hiyo, Emma Oriyo na Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Dorris Malulu.

1 comment:

  1. leo mnachukua michango kutoka kampuni ya bia ? ama kweli dunia adaa.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad