Salam,
Shikamoo
wakubwa na vijana wenzetu mambo vipi? kwanza kabisa tunapenda
kuwashukuru Mabloga wote popote Duniani kwa kuendelea kutusaidia kwa
kiasi kikubwa sana kutufikishia ujumbe wetu pale tunapo omba kusaidiwa,
Baada ya shukrani hizo za kipekee kabisa, Pia tunapenda kuchukua nafasi
hii kuwashukuru wale wanavyuo,watumishi wa vyuo na wadau wote ambao
wameendelea kuipa sapoti kubwa website ya MATUKIO NA WANAVYUO.
Ili kuendeleza kuwaunganisha wanavyuo wote Tanzania na kuwakutanisha na
wanavyuo wengine ambao ni watanzania lakini wanasoma nje ya nchi
tumeamua sasa kuwaletea njia mbadala ambayo itawaunganisha kirahisi
kabisa nayo ni Socilal network.
Hivyo basi kwa heshima na taadhima tunapenda kuwatambulisha kwenu kiunganishi kipya kabisa ambacho kinakwenda kwa jina la UNIVERSITIES CONNECTS .na Jina la tovuti ni www.tzuniversitiesconnects.tk
Katika website hii maalum kabisa wanavyuo na wanafunzi mbalimbali
pamoja na wadau wataweza kukutana humo, kubadirishana mawazo ya kisomi
zaidi na kufahamiana zaidi ikiwa ni pamoja na kupata mawazo mapya, pia
wataweza kupata marafiki wapya na kama haitoshi kuna Visual Discussion
Room ambapo wataweza weka Mada mbali mbali na kuijadili moja kwa moja,
na zaidi ya yote utapata nafasi ya kuchati muda wowote.
Pia kwa
kuzingatia kuwa wanafunzi wengi wanatumia Mobile phones, basi kupitia
Mtandao huu utaweza pia kutumia simu yako ya mkononi kuendelea
kuwasiliana. Ni matumaini yetu ya kwamba mtandao huu wa kipekee na mpya
kabisa utaenda kukuunganisha wewe na mwenzako...
Tunaomba ukipata
taarifa hii umwambie na mwenzako pia ajiunge ni Bure kabisa.
Tunatanguliza Shukrani zetu asanteni sana.
Sisi,
Matukio na wanavyuo Crew
Matukio na wanavyuo Crew
ILI KUJIUNGA MOJA KWA MOJA BOFYA HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment