HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 10, 2011

Mkutano wa wafanyabiashara Afrika Mashariki kufanyika Novemba


Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank Tanzania Jamal Hussein, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya maandalizi ya mkutano wa Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki ambao utafanyika Hoteil ya Fairmont Mt. Kenya Safari Club, Nanyuki nchini Kenya kuanzia tarehe 17 mpaka 20 Novemba mwaka huu. Mada ya mkutano huo itakuwa ‘Ubunifu- chanzo cha ukuaji wa biashara Afrika Mashariki’. Mkutano huo wa Waandishi wa Habari umefanyika leo Septemba 9, 2011 katika Hotel ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
Bw. Salim Bashir, ambaye ni kiongozi wa KPMG Tanzani, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya maandalizi ya Mkutano wa Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki ambao utafanyika katika Hotel ya Fairmont Mt. Kenya Safari Club, Nanyuki nchini Kenya kuanzania tarehe 17 mpaka 20 Novemba mwaka huu. Mada ya Mkutano huo itakuwa ‘Ubunifu- chanzo cha ukuaji wa biashara Afrika Mashariki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank Tanzania. Mkutano huo wa Waandishi wa Habari umefanyikaleo Septemba 9, 2011 katika Hoteli ya Movenpick, Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu.

Maandalizi ya mwaka huu ya mkutano wa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki yameanza ambapo zaidi ya viongozi wa makampuni makubwa 100 katika Ukanda huu wanatarajiwa kushiriki.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kushiriki katika mkutano huo mkubwa ni pamoja na viongozi wa makampuni kutoka Tanzania, Uganda, Rwanda na Kenya na wanamatumaini kwamba biashara zao zitanufaika na ubunifu pamoja na fursa zinazojitokeza katika Ukanda huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti mhamasishaji wa Tanzania, Bw.Jamal Hussein alisema mada ya mwaka huu ni ‘Ubunifu- chanzo cha kuchochea ukuaji wa biashara Afrika Mashariki’ ambapo taasisi na serikali zimeweka jitihada ya kufanya Shirikisho la Africa Mashariki kuwa kivutio cha kukuza uchumi.

Bw. Hussein alisema mkutano huo utafanyika Fairmont Mt. Kenya Safari Club kuanzia tarehe 17 hadi 20 Novemba mwaka huu na huu ni mkutano wa tano kufanyika, na utakuwa maalum kwa kujibu baadhi ya changamoto zinazoathiri biashara katika Ukanda huu na kuzitafutia ufumbuzi .

‘Mkutano wa mwaka huu unalenga kutumia mafanikio yake ya nyuma, na kutafuta njia nyingine za kuendeleza na kukuza fursa zinazojitokeza katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla. Tunataraji kujua na kufahamu jinsi gani mikakati na maamuzi ya viongozi yanaweza kuboresha ukuaji wa biashara’, alisema Bw. Hussein.

Alisema kuwa waandaji wa mkutano ujao (Citibank, Deloitte, KPMG, Nation Media Group, PwC and Serena Hotels) hivi karibuni watataja wazungumzaji wa ndani na wa kimataifa waliochanguliwa kwa kuzingatia uzoefu wao katika ubunifu ili kuongoza mazungumzo wakati wa mkutano.

‘Tutawakutanisha wafanyabiashara wenye uzoefu wa hali ya juu katika Ukanda huu. Lengo ni kushirikisha umma na watu binafsi kwenye bara hili kwa ujumla ili tuweze kuboresha uchumi wa Afrika Mashariki. Tutawataarifu kinachoendelea kadri muda wa mkutano unavyokaribia’, alisema Bw.Salim Bashir mshirika wa KPMG na mjumbe wa kamati ya maandalizi.

Mkutano wa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki ni jukwaa ambalo huwakutanisha viongozi katika nyanja ya biashara Afrika Mashariki na kubadilishana mawazo na maoni juu ya changamoto mbali mbali zinazowakabili na kuangalia namna ya kuzikabili kwa pamoja.

Zaidi ya viongozi 150 wa juu wa makampuni na taasisi muhimu za serikali walihudhuria mkutano wa nne ambao ulifanyika mwaka 2008 Kampala, Uganda chini ya mada: ‘Kukua kwa Ushindani Ndani ya Afrika Mashariki’.

Baadhi ya mambo muhimu yatakayozungumzwa wakati wa mkutano ujao ni pamoja na:

Kuzingatia Ubunifu Katika Uchumi Unaokua, Vyombo vya Habari na Masoko, Kusimamia Kipaji kwa Ubunifu, Kuwezesha Ubunifu (kifedha), changamoto za kisera; Ushirikiano katika sekata za umma na binafsi;,Kushirikisjha Sekta Binafsi Katika Uundwaji wa Sera za Umma, Kufanya Kipaji kupewa kipaombele.

Katika mikutano iliyopita, ikiwa ni pamoja na ule uliofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto nchini Tanzania mwaka 2004, na kuibua mipango mingi inayotekelezeka kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuimarisha mawasiliano ya simu, kukuza kilimo; kushirikiana na mataifa mengine kwa njia ya makubaliano ya miundombinu, na kuanzisha vituo vya utumiaji wa wakala wa biashara. Mafanyikio makubwa kwa sasa ni kuwa na mkongo wa bahari wa mawasiliano Afrika Mashariki.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad