Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando
akifafanua jambo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari juu kupanga ratiba ya
fainali za Taifa za michuano ya Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza
Jumamosi hii kwenye uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume Dar es Salaam,
zikishirikisha timu za kombaini za Mwanza, Iringa, Morogoro na Dar es Salaam.
Pamoja naye ni Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura (katikati ) na Afisa
Mashindano Iddi Mshangama. Upangaji ratiba huo ulifanyika kwenye ofisi za TFF,
Dar es Salaam leo Jumatano Septemba 14, 2011.
Kikosi
cha timu ya mwanza cha vijana chini ya umri wa miaka 17 watapambana vikali na
kikosi cha timu ya morogoro katika mashindano ya kusisimua ya Airtel Rising Star
yatakayoziduliwa na kuchezwa katika viwanja vya karume siku ya Jumamosi Dar es
salaam huku wenyeji kikosi cha timu ya Dar es Salaam kikijiandaa
kuchuana Iringa siku Jumapili
Droo
ya kupanga mechi za fainali ilifanyika Jumatano 14 septemba 2011 katika ofisi
za TFF jijini Dar es Saalam ambapo Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson
Mmbando aliwapa changamoto wachezaji kuonyesha uwezo wao wa kulisakata
kandakanda ili waweze kuonekana na kuchaguliwa na kikosi cha ufundi toka
TFF na kuwa kati ya wachezaji sita bora watakaoingia clinic
Wachezaji
sita bora watapata nafasi ya kuingia katika cliniki itakayoendeshwa na wajuzi
wa soka kutoka manchesta na kupata mafunzo, washindi hao watakuwa kambini na
washiriki wengine kutoka nchi za jirani kama Kenya, Uganda, Malawi and Sierra
Leone. Aliongeza
Zaidi
yawashindi bora watakaochaguliwa mashindano ya Airtel Rising Star yatatoa
zawadi mbalimbali kwa shule zilizoshiriki ikiwemo vitabu vya masomo ya
sekondari ambayo vitawasaidia katika kuinua viwango taaluma mashuleni
Mmbando
aliongeza kwa kusema tunagetemea kupokea timu kutoka mikoani kuanzia Alhamisi,
15 Septemba 2011. Matayarisho ya malazi, chakula na vifaa vya michezo kwa timu
zote yamekamilika
Akiongelea
kuhusu cliniki hiyo ya Manchesta united Mmbando aliongeza kwa kusema, ni
ya kiwango cha hali ya juu na itakayowapatia vijana mafunzo bora na ya kiwango
cha juu ambayo itaanza Rasmi tarehe 30 october 2011 hapa Dar es Saalam.
No comments:
Post a Comment