KUNDI
jipya la muziki wa taarab la Tanzania Moto Modern Taarab (T-Moto)
limetua jijini Dar es Salaam leo asubuhi kutoka mfichoni katika Visiwa
vya Zanzibar, lililokuwa limejichimbia kwa ajili ya maandalizi ya
uzinduzi wake uliosogezwa mbele hadi Oktoba 28 mwaka huu.
Kundi
hilo limewasili jijini baada ya kusitisha mazozi yake kwa muda kwa
ajili ya maombolezo ya msiba wa Meli ya Mv Spice na linatarajia kuingia
studio kwa ajili ya kurekodi nyimbo zake mbili kati ya zilizosalia ili
kukamilisha albamu yao.
Akizungumza
katika Bandari ya jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kundi hilo
Amin Salmin, alisema kwamba kundi hilo litaingia katika stuio za Bakunde
na kurekodi nyimbo sita ambazo zitakamilisha albamu yao iitwayo
‘Aliyeniumba Hajanikosea’.
Aidha
alisema kuwa baada ya kumaliza zoezi la kurekodi nyimbo hizo, kundi
hilo linatarajiwa kufanya ziara katika mikoa ya Tanzania na nchi jirani
ya Kenya, kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kundi na albamu yao Oktoba 28, jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa wasanii wa kundi hilo ambaye ni mkongwe katika muziki huo wa Taarab,
Bi. Mwanahawa Ally alisema anashukuru kambi hiyo imewaweka katika
mwelekeo mzuri ambapo anaamini kazi zitakazotoka zitakuwa na viwango vya
hali ya juu hivyo amewaomba mashabiki wakae mkao wa kula.
“Nataka
niwaeleze mashabiki wa tasnia ya taarab kwamba tunakuja kwa moto kama
lilivyo jina la kundi letu, moto ambao si rahisi kuzimika kwa kijipipa
cha maji, hivyo mashabiki wetu wasubiri mambo mazuri na ya kupendeza
kutoka kwetu, tunawaomba mashabiki watupokee vizuri kwa kujitokeza kwa
wingi katika maonyesho yetu,”Alisema.
Tayari kundi hilo limeshatoa nyimbo mbili ambazo zimeweza kuliwatambulisha vyema.
Nyimbo
hizo ni pamoja na uliobeba albamu hiyo‘ Aliyeniumba Hajanikosea’
ulioimbwa na Mwanahawa Ally, pamoja na ‘Unavyojidhani Mbona Hufanani’
ulioimbwa na Jokha Kassim.
Nyimbo
nyingine zinazotarajiwa kuwamo katika albamu hiyo ni pamoja na ‘Mtoto
wa Bongo’ ulioimbwa na Hassan Ally, ‘Mchimba Kaburi Sasa Zamu yake
imefika’ ulioimbwa na Mrisho Rajab, ‘ Mwenye Kustiri Mungu’, ‘Kumbe Wewe
ni Shoti’ ambazo zimeimbwa na Mosi Suleiman na ule wa ‘ Riziki na
Shortcut’ ulioimbwa na Aisha Masanja.
Kundi
hilo limesheheni wasanii wenye vipaji vya hali ya juu wakiwemo
Mwanahawa Ally, Jokha KAssim, Jumanne Ulaya ‘Mkono wa Biashara’, Mrisho
Rajab, Musa Mipango, Hassan Ally, Mosi Suleiman, Rajab Kondo, Fadhili
Mnara, Moshi Mtambo, Ally Kabura, Sabha, Rahma , Asha Masanja na Hanifah
Kasim na wengineo.
No comments:
Post a Comment