HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 13, 2011

hali ilivyokuwa leo kwenye tamasha la Jinsia 2011 katika viwanja vya TGNP mabibo

Mgeni rasmi wa tamasha la 10 la jinsia,kutoka chuo kikuu,nchini Ghana,Profesa Dzodzi Tsikata akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonesho ya kazi za Wanawake na Wanaharakati,leo kwenye tamasha hilo lililofanyika kwenye viunga vya ofisi hizo,Mabibo jijin Dar na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.Tamasha hilo ambalo msisitizo wake mkuu ilikuwa ni "Jinsia,Demokrasia na  Maendeleo:Ardhi,Nguvukazi na maisha endelevu",likiwa limeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakishirikiana na wanaharakati wa FemAct.
Mgeni rasmi wa tamasha la 10 la jinsia,kutoka chuo kikuu,nchini Ghana,Profesa Dzodzi Tsikata akikabidhiwa baadhi ya vitabu na Dada Sara Ezra kutota banda la UTU .
 Bidhaa mbalimbali zilikukuwepo kwenye tamasha la 10 la jinsia.
 Pichani juu na chini ni wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tamasha la 10 la jinsia,lililofanyika kwenye Ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Mabibo jijini Dar.
Mwanamuziki mahiri wa nyimbo za asili,Vitalis Maembe akiimba jioni ya leo kwenye tamasha la 10 la jinsia.
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye tamasha la jinsia,tamasha hilo la 10 linaendelea tena kesho kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania,Mabibo jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad