Taarifa iliyotufikia mapema leo kutoka huko visiwani Zanzibar,inataarifu kuwa Meli ya MV Spice Islands iliyokuwa safarini ikitokea Unguja kuelekea Pemba imezama katika mkondo wa Nungwi majira ya saa tisa za usiku wa kuamkia leo na kusadikiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 600.
Meli hii ambayo hubeba abiria na mizigo ambayo hufanya safari zake hizo kila siku, inasemekana ilikuwa na abiria 610 waliosajiliwa na hadi hivi sasa inadaiwa ni miili 100 tu iliyofanikiwa kuonekana na bado wataalam wa uokoaji wanaendelea kutafuwa miili mingine.
Mungu aziweke mahala pema peponi roho za ndugu zeru hao.
-Amein
Tutaendelea kujulishana zaidi kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia kutokea eneo la tukio.hivyo tendelee kuvuta subira.
===========================
===========================
Meli
ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko
Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mh Issa Haji Ussi akithibitisha
tukio hilo amesema ajali imetokea milango ya saa 8:30 za usiku wa
kuamkia leo, na kuongezea kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610
pamoja na mizigo.
Mh
Ussi amesema meli hiyo iliyokuwa imeondoka katika Bandari ya Malindi
Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata
hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.
Hadi
sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini
vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.
Naibu
Waziri huyo amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri
vya binafsi vya boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa
msaada unaohitajika, huku Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helikopta
yake kwenye eneo la tukio.
Awali,
amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo
baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika
kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.
Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.
No comments:
Post a Comment