Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imeendelea kuwafikishia wakazi wa nyanda za kusini
huduma za mawasiliano bora na kwa bei nafuu.
Airtel imefikisha
huduma za mawasiliano katika vijiji vipatavyo 20 ndani ya mwezi mmoja vyenye
idadi ya watu wapatao 52,775 ambao kwa kupitia mtandao wa Airtel wataweza
kuboresha shughuli za kilimo , biashara, katika kuinua uchumi wa jamii na
nchi kwa ujumla.
Vvijiji
vitakavyofaidika na huduma hizi ni Kaulolo, Nsenkwa,Mtakuja,Inyonga na Kamsisi
mkoani Rukwa kwa Mkoa wa mbeya ni vijiji vya
OldVwawa,Isangu,Ilolo,Ilembo, Mwantengo,Hasamba,Ukingani Majengo,
Mpangala,Kinyika,Ndapo,Nhungu, Matamba na Mahanji wakati Mkoani Iringa ni
Kibena, Tea estat.
Akiongea kwa
niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano wa kampuni
ya simu ya Airtel Jackson Mmbando alisema” Mawasiliano ni muhimu katika
kuboresha ulinzi, kukuza uchumi, kuweka jamii pamoja na kwa kutambua hilo,
Airtel tumewekeza zaidi katika kupanua huduma zetu za mawasiliano hasa vijijini
ambapo ndiko kwenye changamoto kubwa”.
Airtel
tumeweza kuwafikishia huduma za mawasiliano kwa Wakazi wa maeneo ya
Matamba eneo maarufu kwa shughuli za kilimo na utalii, Pia tumewekeza
kikamilifu na sasa mawasiliano bora yanapatika katika mbuga za KITULO zilizoko
wilayani Rungwe mkoani Mbeya, wataliii sasa wataweza kuwasiliana na ndugu zao
wakiwa katika ziara ya mbuga hizo aliongeza Mmbando.
Airtel
inaendelea kupanua mtandao wake na kuwapatia wateja wake huduma bora na kwa bei
nafuu zinazopatikana nchni nzima, lengo likiwa ni katikati kutimiza
dhamira yake katika kuwafikia wananchi wengi na kuboresha huduma za mawasiliano
nchini hasa katika vijiji mbalimbali nchini
“Mkakati
wetu wa kupanua mawasiliano vijijini unaendelea kwa kipindi chote cha Mwaka huu
lengo letu ni kuhakikisha tunawafikishia wananchi wote huduma ya mawasiliano
yenye utulivu zaidi na kutatoa uhuru wa mawasiliano zaidi kwa wateja
kuendelea kufanya mawasiliano yenye manufaa yatakaowafanya wafurahie
kutimiza miaka 50 ya uhuru wakiwa na miundombinu ya mwasiliano
yanayojitosheleza” alimaliza kusemba Mmbando
No comments:
Post a Comment