HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 21, 2011

Ubalozi Wetu Uingereza wafutarisha

Waalikwa wakiomba dua baada ya kufuturu katika ubalozi wetu London, jana.
Asalaam Aleikhum,

Ubalozi wa Tanzania Hapa London jana uliwaalika watanzania  kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu. 


Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa  katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh Chabaka Kilumanga aliwashukuru wadau wote ambao walioweza  kujumuika na kufuturu kwa pamoja. 


Aidha Mh Kilumanga  aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi kwa hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili ya wote hivyo kila mtu na autumie ipasavyo.

Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.

Asanteni Sana,

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
URBAN PULSE CREATIVE
Naibu Balozi Mh. Chabaka Kilumanga akitoa shukrani  na neno kwa waalikwa
Sehemu ya wageni
Afisa ubalozi Bw. Zamarani akikaribisha wageni kufuturu
Baadhi ya waalikwa kinama wakifuturu
Mkuu wa utawala na fedha ubalozini hapo Da'Carol Chipeta (shoto) akipozi 
na Da' Jestina George

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad