HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 25, 2011

Mgogoro wa Ardhiwafukuta Kipera Wilayani Mvomero,wananchi waitakaserikali ya wilaya na mkoa kuingilia kati haraka

Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kuhusu kubomolewa choo chake na kuwekwa kwa uzio wa seng’enge na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa  Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa jana Kijijiji hapo
Baadhi ya Wananchi wa Kitogoji cha  Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakipita  pembezoni mwa uzio wa senyeng’e iliowekwa na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa  Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa jana Kijijiji hapo.
Mkazi wa Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Ally Kidunda, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliokuwa uzikutanishe pande mbili za wakulima wa kijiji hicho na mzungu anayemiliki kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayodai kununua shamba katika kityongoji cha Kinyenze na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia ya kwenda mtaa wa Mwanga. (Picha na Mroki Mroki).
Na Mroki Mroki, Mvomero

WANANCHI waKitongoji cha Kinyenze , Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali , Wilaya ya Mvomeromkoani Morogoro wamewataka viongozi Wilaya na Mkoa huo kuingilia kati harakamgogoro wa ardhi baina yao na mwekezaji wa Kigeni aliyeuziwa shamba kijijinihapo.

Wananchi hao pia wamewashutumubaadhi ya Viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwakushindwa kutatua mgogoro wa muda mrafuwa mipaka ya ardhi kati ya Kijiji na Mwekezaji Raia wa Kigeni mmiliki waKampuni ya Tanbreed Poultry Limited aliyeuziwa shamba kijijini hapo.

Wakizungumza kwanyakati tofauti kwenye mkutano wahadhara ambao ulipangwa kuzikutanisha pande mbili hizo zenye mgogoro wa mipakaya ardhi chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo na maofisa wake wa Idara ya Ardhi ili kufikiamuafaka wa sakata hilo, wakazi hao wameulamu Uongozi wa Halmashaurikwa kushindwa kutokea mkutanoni hapo namwekezaji huyo.

“Kitendo cha Viongozikupanga tarehe na kushindwa kufika bila sababau maalum ni dharau kubwa kwetuwananchi na endapo tatizo tulilonalo halitashughulikiwa haraka, sisi tutachukua maamuzi yetu wenyewe yakubomoa uzio uliowekwa na muwekezaji huyo na lolote litokee”, alisema ShabanMaguo.

Viongoziwaliopaswa kufika katika mkutano huo lakini hawakufika ni Pamoja na Mkurugenziwa Halmashauri ya Wilaya ya Mvovero, Maofisa wa Ardhi, Ofisa Mtendaji wa Kijijicha Kipera, na Ofisa Mtendaji wa Kata aliyefika na alipoona waandishi wa habarialitoweka bilakuaga.

Wananchi haowalishagazwa kuona Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, ambao waliandikabarua ya kuutaka Uongozi wa Serikali ya Kijiji kuitishwa mkutano wa pamoja wapande hizo, Agosti 23, mwaka huu , lakini walishindwa kutokea pamoja na Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji pamojana Mwekezaji huyo ambaye ni Mmiliki wa Kampuni ya Tanbreed Poultry Limitedinayomilikiwa na Mzungu.

Mkazi waKitongoji hicho ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji chaKipera, Ally Kidunda, alidai kuwa kushindwa kutokea kwa viongozi hao ambaowenyewe ndio walioandika barua nakuopanga siku ya mkutano huo, kinawatia wasi wasi juu ya kutaka kuficha ukweliwa mambo.

“ sisi hatuna imani na Viongozi wetu , kamawao ndiyo wameandika barua yenye kumbukumbu namba MVDC /V.10/4/12 ya Agosti 4,mwaka huu na kutaja tarehe 23 mwezi huu ni siku ya kufanyika mkutano wa pamojawa mgogoro wa shamba namba 296 Kinyezi , Kipera, Wilaya ya Mvomero, lakiniwameshindwa kutokea” Kidunda alishangazwa na jambo hilo.

Naye mkazi waKitongoji hicho, Said Ahamad , alisema ,wakazi wa kijiji hicho ni watu wanaheshumu sheria , na kufyata utaratibu wakutatua mingigoro, lakini itafikia wakati wananchi watashindwa kuwa nauvumilivu , kitendo ambacho wanadiriki kujichukulia sheria mkononi , jamboambalo ni hatari kwa amani na utulivu.

Nao HadijaMwinyipembe, na Mwajabu Shaabani, wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Mkutano huo, walidai kuwa uzio uliowekwa na kampuni hiyo ya TanbreedPoultry Limited umefunga njia kuu iliyokuwa ikitumiwa kwenda katika mashambayao, kisima cha maji pamoja kukata mawasilino baina ya kitongoji chao na mtaawa Mwanga ambao unakaya zaidi ya 100 na huduma za kijamii wanazipata hapoKinyenze.

Kufungwa kwa njiahiyo kunasababisha mazao kuharibikia shambani zikiwemo nyanya, na pia mazaomengine ya kudumu kama miwa na minazi imekuwa ikivunwa na walinzi wa shambahilo.

Kwa upande wakeBibi Mawazia Kibwana, alidai kuwa katika zoezi hilo , amebomolewa Choo chake nakusababisha kupata shida ya kujisaidia hasa nyakati za usiku jambolinalomlazimu kujisaidia katika ndoo.

Naye Mkazi waKitongoji hicho mtaa wa Mwanga, Mary Nathan, alisema kufungwa kwa njia zotezinazokwenda katika makazi yao kunasababisha watoto kutokwenda shule hatawagonjwa kupata usumbufu mkubwa.

Mwenyekiti waSerikali ya Kijiji cha Kipera, Karoli Anthoy, alisema Machi 28, mwaka huuMwekezaji huyo alifika Ofisi ya Kijiji kwa ajili ya kujitambulisha kuhusukununua shamba lililolopo katika eneo la Kijiji alilouziwa na mwananchimmoja

“ Uongozi waserikali ya kijiji ukaanza kuona harakati za uwekaji wa uzio , katika zoezihili Serikali ya Kijiji haikushirikishwa , imewekwa na mwekezaji pekee ,kitendo kilichozusha matatizo baada ya kuingilia maeneo ambayo si mali yake”alisema Mwenyekiti huyo

Alisema kutokanana kutokea kwa mgogoro huo, Serikali ya Kijiji imeamua kuunda kamati yakushungulikia suala hilo katika ngazi ya Wilaya na Mkoa , ambapo hadi sasa badomajawabu hayapatikana kitendo kinachozidisha hasira za wananchi dhidi yamwekezaji huyo.

Kwamujibu wawakazi hao wanadai kuwa eneo lililoingiliwa na mwekezaji huyo wa kigeni liponje ya mipaka ya shamba alilonunua na mwaka 1997 paliwahi kuwa na mgogoro tenana Mahakama ya Wilaya kutoa hukumu kuwa eneo wanaloishi na kulima wananchi haolipo nje ya mipaka ya shamba la Badru Walji ambalo limeuzwa kwa TanbreedPoultry Limited kampuni inayomilikiwa na mzungu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad