Na Hamad Hija - Maelezo Zanzibar.
Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) jana limetangazsa kuwepo kwa mgao wa dharura wa Umeme kutokana na kuharibika kwa moja ya Transfoma kubwa inayosambaza umeme iliopo kituo cha Umeme Mtoni wilaya ya Magharibi Unguja.
Afisa uhusiano wa Shirika hilo Bw Salum Abdulla Hassan amesema kuwa kufuatia kuharibika kwa Transfoma hiyo hapo Mtoni itakuwa vigumu kwa Transfoma iliobakia kuweza kubeba mzigo wa matumizi katika maeneo yote ya Unguja.
Bw Hassan amefahamisha kuwa mgao huo utaendelea usiku na mchana hadi hapo matengenezo ya Transforma yatakapomalizika.
Amesema mgao huo wa dharura utahusisha zoni zote isipokuwa ile ya Fumba ambapo kila zoni itapata umeme saa nane na kukosa mawili.
Ofisa huyo wa Uhusinao wa ZECO bwana Salum amewataka wananchi kuwa wastahamilivu kufuatia tukio hilo la dharura na hali itarudi kuwa ya kawaida baada ya tatizo hilo kutatuliwa.

No comments:
Post a Comment