Marehemu Coster Mowo enzi za uhai wake
Mpendwa wetu COSTER MOWO tarehe 19/8/2011 unatimiza mwaka mmoja toka ulipo tuacha ghafla na kuiacha familia yako kwenye giza nene,hakika machoni tunaonekana tukichoka mioyo yetu daima bado inasononeka.
Tunakukosa sana japo tunaelewa wakati wote wewe ni sehemu ya maisha yetu na upo mioyoni mwetu. Tunaendelea kukuombea,unakumbukwa sana na mkeo kipenzi,wazazi wako,watoto wako,ndugu,jamaa,marafiki zako na uongozi mzima wa flavanite. Roho yako ipumzike kwa amani daima.
Kutakuwa na misa ya kumbukumbu tarehe 19/8/2011 nyumbani kwao kiboroloni,moshi.


No comments:
Post a Comment