Meneja wa duka la Vodacom la Mlimani city Fatuma Kalyanye akiwaonyesha baadhi ya warembo wanaoshiriki katika kinyanganyiro cha miss Temeke baadhi ya bidhaa zinazouzwa katika duka hilo,Warembo wa kitongoji hicho walitembelea ofisi za Vodacom Tanzania kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na wadhamini wakuu wa shindano hilo,wengine kushoto ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa,akiongea na baadhi ya washiriki wa Miss Temeke walipotembelea makao makuu ya Vodacom Tanzania kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali katika kampuni hiyo wakiwa ni wadhamini wakuu wa shindano la Miss Temeke litakalofanyika hivi karibuni.
Mtaalam wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu kushoto akiwaongoza baadhi ya washiriki wa MissTemeke walipofika kutembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani city kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo,Vodacom ndiyo wadhamini wakuu wa shindano la Miss Temeke litakalofanyika hivi karibuni.
Mtunza nyaraka muhimu za wateja wa Vodacom Tanzania James Oswin akiwaelekeza baadhi ya warembo wa kitongoji cha Temeke namna ya kujaza fomu za kujiunga na huduma ya Mpesa warembo hao walitembelea ofisi za Vodacom Tanzania ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali hapo jana.
No comments:
Post a Comment