Mkurugenzi wa Ununuzi na Shughuli za kitaalam bi. Lucy Nderimo akitoa mada iliyohusu mfumo wa ugavi wa bohari kuu ya dawa ambapo manunuzi yote yanafanyika kwa kuzingatia sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005.
Mkurugenzi wa mahusianao ya wateja na uendeshaji wa kanda toka msd, bw. Cosmas Mwaifani akitoa mada iliyohusu miaka 17 ya MSD,ufanisi na changamoto (1994-2011).Alitaja changamoto zinazoikabili bohari hiyo ni pamoja na ile ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vya umma kwenye maduka na vituo vya afya vya watu binafsi na uchache wa viwanda vya ndani katika sekta ya uzalishaji dawa na vifaa tiba ambao unakidhi mahitaji ya nchi kwa asilimia 20 tu.
Katibu Mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii bi. Blandina Nyoni, akisoma hotuba kwenye semina ya wabunge kuhusu majukumu ya bohari kuu ya madawa nchini.
No comments:
Post a Comment