HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 9, 2011

TIMU NYINGI ZAJITOKEZA KUSHIRIKI MASHINDANO YA SAFARI LAGER POOL

Haji Omary wa timu ya Mkwajuni akicheza wakati wa mashindano Pool Safari Lager dhidi ya mpinzani wake Omary Timbuli wa Ubungo wakati wa mashindano hayo
Nelson Mtenda wa timu ya Madrid akicheza dhidi ya mpinzani wake Stanford Mwakajila wa timu ya Mlalakuwa wakati wa mashindano hayo.

MASHINDANO ya Pool Safari Lager katika hatua za awali Shoko na Topland zaonyesha ubabe wa kuongoza mashindano hayo katika Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Timu ya Shoko yenye makazi yake Mbezi Beach inaongoza kundi A, mara baada ya kuzifunga timu zote za kundi hilo wakati wa mashindano hayo kwa kucheza michezo minne na kushinda yote ikifuatiwa na Meeda ambayo inamichezo 4,imeshinda 3 na kupoteza 1.

Timu zingine ni Mkwajuni inamichezo 3,imeshinda 1 na imepoteza 2,Ubungo inamichezo 3,imeshinda 1na kupoteza 2 na Jaba ina michezo 4 na imepoteza yote.

Wakati kundi B, Topland yenye makazi yake pale Mikumi jijini Dar es Salaam inaongoza kundi hilo ambapo inamichezo 4,imeshinda 3 na imepoteza 1,ikifuatiwa na 4Ways ambayo imeshinda michezo 2 na kupoteza miwili.

Timu zingine katika kundi hilo ni Bahama ambayo imeshinda michezo 3, imepoteza 2,Madrid inamichezo 3,imeshinda 1na imepoteza 2 na Mlalakuwa inamichezo 3,imeshinda 1na imepoteza 2.

Katika hatua za wawali timu mbili zinatakiwa kuondoka na timu 8 kuingia hatua ya robo fainali.

Mashindano hayo yanafanyika katika Klabu ya Mwanese Mabibo jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa TBL kupitia bia ya Safari Lager.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad