Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwte akiteta jambo na Katibu Uenezi na Itikadi CCM Nape Moses Nnauye wakati wa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Chama Cha TANU zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana usiku.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wanachama wa CCM waliohudhuria maadhimisho ya kuzaliwa Chama Cham TANU zilizofanyika katika makao makuu ya CCM na baadaye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana usiku .Kushoto ni mkewe Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais mama Salma Kikwete akishiri kuimba wimbo maalum wa sherehe za kuzaliwa TANU pamoja na wasanii wa bendi Vijana CCM wakati wa maadhimisho ya kuzaliwa Chama cha TANU zilizofanyika katika katika viwanja vya Mnazi mmoja jana usiku jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuwasha taa maalum kuashiria uzinduzi wa sherehe za kumbukumbu ya Kuzaliwa chama cha TANU mnamo mwaka 1954,zilizofanyika jana katika ofisi kuu ya CCM,Mtaa Lumumba jijini Dar es Salaam jana usiku na baadaye sherehe za mkesha katika viwanja vya mnazi mmoja.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara),Pius Msekwa (kushoto),Katibu Unezi na Itikadi CCM Nape Nnauye (pili kushoto),Katibu Mkuu wa CCM,Wilson Mkama pamoja na mjumbe wa CCM wakifatilia hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM,Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na muasisi wa Chama cha TANU mzee Constantine Milinga wakibonyeza kitufe maalum jana kushiria siku na saa ambapo chama cha TANU kilipozaliwa Tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 1954.Wengine katika picha kutoka kushoto ni katibu mwenezi CCM Taifa Nape Nnauye, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mkama.
Kapten John Komba akiongoza safu yake katika kunogesha sherehe hizo kwa kwaya nzuri kabisa.
Kapten John Komba akiongoza safu yake katika kunogesha sherehe hizo kwa kwaya nzuri kabisa.
umati mkubwa wa watu ulihudhulia katika sherehe hizo za kukumbuka kuzaliwa kwa TANU.
No comments:
Post a Comment