Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah (pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na washiriki wa Redd's Miss Temeke (hawapo pichani) leo wakati wa ziara ya warembo hao kwenye kiwanda cha bia cha TBL.kulia ni Mratibu wa shindano hilo la Redd's Miss Temeke,Benny Kisaka na kushoto ni Meneja Mahusiano wa TBL,Edith Mushi pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's,Victoria Kimaro.
Mtengenezaji wa bia za TBL,Elisanguo Metha (kushoto) akiwapa maelekezo baadhi ya warembo watakaoshiriki Redd's Miss Temeke 2011 wakati walipotembelea kiwanda cha bia zinazotengenezwa na kampuni ya bia Tanzania leo.
Warembo wa Redd's Miss Temeke 2011.
WAREMBO wa Miss Temeke wametakiwa kujiheshimu kwa kuwa fani ya urembo sio ya kukimbilia kusaka umaarufu kwa tabia chafu na kudhalilisha fani hiyo na familia kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butalah wakati warembo hao walipofanya ziara ya kutembelea Kampuni hiyo ya bia na kuangalia uzalishaji wa bia na ikiwa ni pamoja na kujifunza masuala mbali mbali ya uendeshaji ndani ya kampuni hiyo.
"Kikubwa tunataka mjiamini na muwe mabalozi wazuri ukizingatia Redd's ndio wadhamini wenu wakuu, hatutaki mtuaibishe au mtutie doa baada ya mashindano mkaanza kuuza magazeti kwa tabia chafu, fani hii sio kimbilio la wenye tabia chafu, mjiheshimu."alisema Butalah na kuongeza
"Fani hii inavishawishi vingi sana, kuweni makini jiheshimuni na mlinde heshima yenu na familia zenu hakuna mzazi ambaye angependa kusoma habari mbaya za mtoto wake, urembo ni kujiheshimu, kujipenda, kujiamini, nidhamu iwe ndio silaha yenu muhimu."alisisitiza
Shindano la Miss Temeke limepangwa kufanyika Jumamosi ijayo Julai 16 kwenye ukumbi wa TCC Chang'ombe huku warembo 15 watashindana katika kinyang'anyiro cha Miss Temeke.Taji la Miss Temeke linashikiliwa na Geneviva Mpangala ambaye pia ni Miss Tanzania anayemaliza muda wake mwaka huu.
No comments:
Post a Comment