Wakongwe wa muziki wa dansi, Nasibu "Ras Nas" (kulia) na Mwanukuzi na Dekula "Vumbi" Kahanga wakiwasha moto mkali kwenye tamasha la Mela lililofanyika Oslo. "Vumbi" mwenye makao yake Stockholm, Sweden, alipiga na bendi ya Ras Nas kama mwalikwa rasmi. Tamasha la Mela mwaka huu limefanyika kwa siku moja badala ya siku nne kutokana na mauaji ya kinyama yaliyofanyika Oslo hivi karibuni. Shoo hii ya Mela ilihudhuriwa na umati wa watu takribani 40,000. Wasanii wengine waliokuwepo ni pamoja na Ky-Mani Marley, Maryam Mursal, Linton Kwesi Johnson na Sain Zahoor.
Madansa wa bendi ya Ras Nas wakifanya wakionyesha umahiri wao wa kucheza mbele ya umatu mkubwa uliofika kwenye tamasha la Mela lililofanyika mjini Oslo.
Shukrani kwa mashabiki ikitolwewa na wanamuzi Ras Nas na Dekula Kuhanga pamoja na wanamuziki wengine.
Nyomi la Maana lililojitokeza kwenye shoo ya tamasha hilo.
sweden hakuna mji unaoitwa oslo,oslo ni norway
ReplyDelete