HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 27, 2011

Mh. Simbachawene afungua fainali za Mchezo wa Pool Taifa leo Mkoani Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Kibakwe,Mh. George Simbachawene akipiga mpira wa mchezo wa pool kwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa fainali za Taifa za mashindano hayo,katika ukumbi wa Kilimani Club,Mjini Dodoma leo.wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa Mchezo wa Pool pamoja na waamuzi.
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Fainali za Mchezo wa Pool Taifa,Mbunge wa Jimbo la Kibakwe,Mh. George Simbachawene akisisitiza jambo kwa wachezaji wa Mchezo wa Pool wanaoshiriki fainali za Taifa wakati akiwahutubia leo kwenye ukumbi wa Kilimani Club,Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Mchezo wa Pool Taifa,Freddy Mushi (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano za mchezo wa Pool kwa ngazi ya Taifa kwenye ukumbi wa Kilimani Club,Mjini Dodoma leo.
Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mkoa wa Dodoma, Nick Tesha akizungumza wakati wa ufunguzi huo.
Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Failali za Mchezo wa Pool Taifa,Mh. George Simbachawene
Baadhi ya Wachezaji wa Pool walioingia kwenye Fainali ya Taifa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
Baadhi ya Viongozi wa Mchezo Wa Pool wakiwa tayari kufuatilia mashindano.
Baadhi ya Wachezaji wakiingia ukumbini.

Na Mwandishi Wetu,Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma ambaye pia ni mwenyekiti wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Simbachawene ameitaka serikali kuutambua mchezo wa pool kama ilivyo michezo mingine.

Mbunge huyo aliyasema hayo leo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa fainali za taifa za mashindano ya mchezo wa pool yanayojulikana kama ‘Safari Lager Nationa Pool Championship 2011’.

Fainali za mashindano hayo zinazoshirikisha mikoa 14 ya Tanzania Bara ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya bia ya TBL kupitia kinywaji chake cha Safari Lager zinafanyikia kwenye ukumbi wa Kilimani Club mkoani hapa.

Simbachawene alisema kuwa awali kulikuwa na dhana ya kuwa mchezo wa pool ni mchezo wa wahuni hadi serikali ikawa inafikiria kuuzuia lakini dhana hiyo haipo tena hivyo serikali haina budi kuupokea na kuutambua kama ilivyo michezo mingine.

“Naiomba serikali kuanzia sasa iutambue mchezo wa pool kama ilivyo michezo mingine kwani ni mchezo mzuri ambao unashirikisha watu wenye heshima zao ikiwemo hata sisi wabunge ambao wiki iliyopita tuliucheza na kuufurahia,”alisema Simbachawene.

Aliongeza kwa kukitaka chama cha mchezo huo nchini (TAPA) kuhakikisha kinausajili mchezo huo kwa kutumia sheria ya mchezo wa ridhaa badala ya kuusajili kama mchezo wa kamari.

“Mchezo wa pool ni mchezo wa kutumia akili na viwango, hivyo TAPA msajili mchezo huu kwa kutumia sheria ya mchezo wa ridhaa badala ya kuusajili kwa sheria ya mchezo wa kamari na wanaotaka kucheza michezo ya kubahatisha (kamari) waende kwenye klabu za usiku,”alisema.

Aidha aliipongeza kampuni ya bia ya Tanzania TBL kupitia bia ya Safari Lager kwa kuweza kuupatia mafanikio makubwa mchezo huo kutokana na udhamini wao .

Naye mwakilishi wa kampuni ya TBL mkoani Dodoma, Niki Tesha alisema kuwa mafanikio ya mchezo huo yametokana na kampuni hiyo kudhamini michezo nchini.

“Kampuni ya TBL inadhamini na kujali michezo nchini na ndiyo maana mchezo huo ambao zamani ulikuwa ukibezwa umeweza kupiga hatua na kufikia hapa ulipo,”alisema Tesha.

Ufunguzi wa fainali hizo ulihudhuriwa pia na Afisa michezo mkoa wa Dodoma,Patrick Ernest pamoja na Afisa Utamaduni wa mkoa huo, Abuu Layya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad