HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 20, 2011

Mafunzo ya walimu wa awali yaliyotolewa na kampuni ya uchapishaji wavitabu nchini ya Long man

Muwezeshaji wa Kampuni ya Pearson Long Man Tanzania inayojihusisha na uchapaji wa Vitabu vya shule za awali na vyuo nchini, Maria Ellokelo,akitaoa mafunzo kwa walimu waliohudhria mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji wa shule za awali jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji wa Walimu wa shule za awali katika shule za Msingi jijini Dar es Salaam,wakijadiliana katika mafunzo hayo yaliyotolewa na Kampuni ya kuchapisha vitabu nchini ya Pearson Long Man.Jumla ya Walimu 90 wanapata mafunzo hayo.
Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Upendp iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam wapili (kulia) akijibu swali wakati wa mafunzo ya uwezeshaji wa Walimu ,kutoka kwa Muwezeshaji wa Kampuni ya Pearson Long Man Tanzania inayojihusisha na uchapaji wa Vitabu vya shule za awali na vyuo nchini, Maria Ellokelo, ali yeshika karatasi kushoto ni Ofisa Mauzo wa Long Man Salama Hamza na Mwalimu wa Shule ya Mkamba ya Temeke Jayneth Gideon.
Ofisa mwandamizi wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Long Man Tanzania inayojihusisha na uchapaji wa Vitabu nhini Belinda Mafuru akimfafanulia jambo Mratibu wa Elimu ya Awali Clarence Mwinuka wa Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi wakati alipohudhuria katika Mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji wa Walimu wa shule za awali na shule za Msingi jijini Dar es Salaam yaliyodhamniniwa na Long Man Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Uwezeshaji wa Walimu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam,wakijifunza kwa Vitendo katika mafunzo yaliyowashirikisha jumla ya Walimu 90 yakiwa yamedhaminiwa na Kampuni ya Uchapishaji wa Vitabu Nchi ya Pearson Long Man.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Uwezeshaji wa Walimu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam,wakijifunza kwa Vitendo katika mafunzo yaliyowashirikisha jumla ya Walimu 90 yakiwa yamedhaminiwa na Kampuni ya Uchapishaji wa Vitabu Nchi ya Pearson Long Man.
Mmoja wa Walimu kati ya 90 waliohudhuria mafunzo ya siku tatu ya Uwezeshaji wa walimu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam,Getruda John kushoto akimwonyesha Mratibu wa Elimu ya Awali Clarence Mwinuka wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa pili kulia na Ofisa mwandamizi wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Long Man,Belinda Mafuru mafundho hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Uchapishaji wa vitabu nchini ya Pearson Long Man.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad